GET /api/v0.1/hansard/entries/587954/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 587954,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587954/?format=api",
    "text_counter": 63,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mabaya yaliyotokea wakati ule yawe funzo kuzuia mengine ya namna ile yasitokee. Mungu ni mwema kwamba mwafaka ulipatikana na Kenya imepata amani. Ushirikiano wetu haukuishia hapo. Hii ndio maana kila wakati kukitokea tukio la ugaidi – watu wanapouawa au kuumia – huwa ninampigia Rais simu kumpa pole. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama – Intelligence Services and Police Force – vina ushirikiano wa karibu kwa sababu wakati mwingine wale watu wakishafanya hujuma huku wanakimbilia kwetu. Lakini tunauliza kimya kimya hatusemi na mtu maana wengine watakuja kusema tunavunja haki za binadamu. Tunauliza kimya na wanakwenda kwa taratibu za kawaida za kimahakama. Nilichokuwa nasemna ni kwamba, tumeweka msimamo wa nchi zetu sisi. Hakuna mtu atakayefanya uhalifu Kenya akadhani kwamba Tanzania ndiyo mahali pa kukimbilia. Hakuna mtu atakayefanya uhalifu Tanzania, akadhani Kenya ndiyo mahali pa kukimbilia. Hivi karibuni, kuna watu fulani hivi walifanya madudu kule, walikuwa wanataka kukimbilia Somalia hawakuwahi kuvuka mpaka; Kenya ikatuambia kuna watu wenu hapa. Katika taratibu zetu za kawaida, tumeshirikiana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}