GET /api/v0.1/hansard/entries/587958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 587958,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587958/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "dawa za kulevya, matumizi ya dawa na biashara ya dawa za kulevya. Imekuwa tatizo kubwa sana sasa. Tunashirikiana kwa pamoja kama vile majambazi wakiiba kule na wakimbilie huku na wakiiba huku wakimbilie kwetu. Hili ni tatizo la pamoja. Tatizo sasa limekuwa ni la dunia nzima. Kila palipo na kifaru ama ndovu, wanasakwa kwa udi na uvumba wauwawe ili pembe zao zichukuliwe wakafanyie biashara. Tumeshirikiana kwa pamoja pia; wale tunawajua kule tunawarudisha, wanaofanya uhalifu huo kutoka kwetu nao tumesaidiana. Katika maswala ya kiuchumi na kijamii, tumekuwa na ushirikiano mkubwa na wa karibu kwa miaka mingi. Katika ujenzi wa miundo mbinu, tumekuwa tukishirikiana kujenga barabara kwa pamoja hasa barabara ya Athi River-Namanga-Arusha ni mradi tuliotengeneza kwa pamoja, tukaomba pesa kwa pamoja; Kenya ikapata mkopo wa kuendeleza upande wake na Tanzania ikapata mkopo kutengeneza upande wake. Jiwe la msingi tuliweka kule Arusha lakini sherehe za kuzindua ile bara bara tulizifanyia Athi River kwa sababu ni mradi mmoja. Hivi sasa tuko na mradi wa pamoja, tunajenga barabara kutoka Arusha mpaka Mwatate lakini later Arusha–Voi Road. Kutoka Mwatate mpaka Voi, barabara ya lami ipo. Nilipokuja ziara yangu hii, Jumapili kazi ya kwanza tulifanya na Rais Uhuru Kenyatta ni kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa bara bara hiyo kwa upande wa Kenya na tunatafuta tarehe tutakayokubaliana wote tutakwenda kufanya vivyo hivyo kwa upande wa Tanzania. Tumekuwa na ushirikiano mkubwa katika ile miradi ya barabara na tuna mradi mmoja, ni wito wa Afrika Mashariki kujenga barabara ya lami kutoka Lamu- Mombasa-Tanga-Pangani-Bagamoyo kwetu sisi mpaka Dar-es-Salaam."
}