GET /api/v0.1/hansard/entries/587988/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 587988,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587988/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hazitakuja pamoja, uwezo wetu wa kushindana katika masoko hata ya kanda zaidi ya Afrika Mashariki au duniani utakuwa mdogo sana. Sisi wakati wote tutaunga mkono ajenda ya utangamano ya Afrika Mashariki na tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba ajenda hiyo inatekelezwa kama vile tulivyokubaliana. Linalotia faraja kama katika mazungumzo na Rais Uhuru na viongozi wengine wa Kenya, moyo wa Kenya nao ni huo huo. Jumuiya ya Afrika Mashariki ndio chombo chetu na sote tukisaidie kiweze kustawi na kufanikiwa."
}