GET /api/v0.1/hansard/entries/588064/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588064,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588064/?format=api",
    "text_counter": 56,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nilifanya hivyo kwa sababu ya umuhimu na nafasi ya Kenya katika diplomasia ya Tanzania. Kenya ina nafasi maalum kwenye diplomasia ya Tanzania. Kenya ni rafiki mkubwa wa Tanzania. Ni mwenza mkubwa katika siasa na medani ya kidiplomasia. Uhusiano wetu ni mkubwa sana. Tunaelewana katika masuala mbalimbali kati ya nchi zetu, masuala yanayohusu ukanda wetu, bara letu la Afrika na masuala yanayohusu dunia. Tumekuwa tukisaidiana kwa pamoja. Wanadiplomasia wetu wanafanya kazi pamoja sio tu kuendeleza masilahi ya nchi zetu mbili, lakini pia kuhakikisha kuwa masilahi ya Afrika Mashariki na bara la Afrika yanaendelezwa. Baina ya nchi zetu tumekuwa tukisaidiana. Matatizo yale yaliyotokea kibahati mbaya baada ya uchaguzi wa 2007, sikusubiri kuitwa lakini niliomba kuja."
}