GET /api/v0.1/hansard/entries/588071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 588071,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588071/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Hon. (Dr.) Kikwete): Ndivyo demokrasia ilivyo. Hata sisi kule, tuliokuwa nao sasa wako upande wa pili, na ndiyo maisha ya siasa. Pili, akasema ananiomba nisiondoke. Lakini nikamwambia nami nina nchi ya kuongoza na hapa Kenya, hapawezi kuwa na marais wawili, kwani hapatoshi. Lakini nilielewa na baada ya pale, ndiyo tukaanza kusaidiana kwa pamoja na iliyobaki ni historia. Sitaki kuyaeleza kusema nilifanya mikutano kwanza na nani? Kwanza, nilifanya mkutano na Mhe. Raila, na nimeambiwa yuko hapa juu."
}