GET /api/v0.1/hansard/entries/588076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 588076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588076/?format=api",
"text_counter": 68,
"type": "speech",
"speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mpaka tukafika mahali tukaelewana. Mwafaka ukapatikana - kwa lugha ya kule kwetu. Tukatoka pale nje tukakutana na wakubwa wale wakatia sahihi. Kenya ikapata mwelekeo mpya wa kisiasa. Kenya mpya ikazaliwa ya Wakenya wanaopendana bila kubaguana. Ningewaomba muendelee na mwelekeo ule ule. Yale mabaya ambayo yalitokea wakati ule yawe fundisho kuzuia mengine ya namna ile yasitokee. Mungu ni mwema, mwafaka ukapatikana na Kenya imeweza kupata amani. Lakini ushirikiano wetu haukuishia hapo ndiyo maana kila wakati kukitokea tukio la ugaidi watu wakiuawa na wengine wakiumia, huwa nampigia Rais simu na kumpa pole. Vyombo vya ulinzi na usalama (Intelligence Services and Police Force) vya nchi zetu mbili vina ushirikiano wa karibu. Wakati mwingine, wale watu wakishafanya hujuma huku wanakimbilia kwetu.Na sisi tukiwajua tunawakamata. Lakini tunawarudisha kimya kimya tu. Hatusemi na mtu. Maana wengine watakuja kusema tunavunja haki za kibinadamu. Yameisha hayo."
}