GET /api/v0.1/hansard/entries/588080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588080,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588080/?format=api",
    "text_counter": 72,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hakuna mtu atakayefanya uhalifu Tanzania akadhani Kenya ndio mahali pa kukimbilia. Hivi karibuni kuna watu fulani hivi walifanya madudu kule, walikuwa wanataka kwenda kukimbilia Somalia lakini hawakuwahi kuvuka mpaka. Kenya ikatuambia, “Bwana, tunao watu wenu hapa.” Katika taratibu zetu za kawaida zile zile tumeshirikiana. Nayasema haya lakini pengine nimesema mengi sana lakini kuna ushirikiano wa karibu sana. Na wakati mwingine tukiyapata sisi tunawaarifu wenzetu na tumeweza kabisa kuokoa mazingira. Kulikuwa na tukio moja, watu walikuwa wanataka kulifanya jambo moja mbaya sana kabla uchaguzi uliopita lakini tulipowajua, tukasadiana na wenzetu wa Kenya tukawakamata wale watu. Kwa hivyo, tumekuwa tunasaidiana sana. Siyaimbi haya lakini hata kwa hivi sasa ushirikiano wetu ni mkubwa sana na ni wa karibu sana."
}