GET /api/v0.1/hansard/entries/588084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588084,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588084/?format=api",
    "text_counter": 76,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hivi sasa tuna mradi wa pamoja. Tunajenga barabara kutoka Arusha mpaka Mwatate. Tunaiita Arusha -Voi Road. Kutoka Mwatate mpaka kule Voi barabara ya lami ipo. Nilipokuja ziara yangu hii jumapili, kazi ya kwanza tumefanya na Rais Uhuru Kenyatta ni kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo kwa upande wa Kenya. Na tunatafuta tarehe tutakayokubaliana wote ili tufanye hivyo hivyo kwa upande wa Tanzania. Tumekuwa na ushirikiano mkubwa katika hiyo miradi ya barabara. Tuna mradi mmoja wetu wa pamoja Afrika Mashariki kujenga barabara ya lami kutoka Lamu, Mombasa, Tanga, Pangani, Bagamoyo kwetu sisi mpaka Dar es Salaam. African Development Bank nayo imekubali kutusaidia kujenga mradi huo. Taratibu sasa hivi zinatengenezwa, nadhani baada ya muda si mrefu nao huo mradi utaanza."
}