GET /api/v0.1/hansard/entries/588088/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 588088,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588088/?format=api",
"text_counter": 80,
"type": "speech",
"speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ushirikiano wetu wa kwanza ni kama nchi zetu mbili zimekubaliana. Kama upande mmoja una umeme, na upande mwingine hauna, hawa watu wa upande huu ambao hawana, wanayo haki ya kupata umeme kutoka kule upande ule wa pili. Tumefanya hivyo kwa umeme. Nyinyi Kenya mumefikisha umeme Namanga. Sisi upande wa Tanzania umeme bado haujafika. Kwa hiyo, Namanga upande wa Tanzania na mji wa karibu wa Longido tumeunganishia umeme kutoka Kenya. Tumefanya hivyo kwa upande ule wa Sirare kule kwetu Tarime. Sisi tuko na umeme. Upande wa pili haukuwa na umeme. Tumechukua umeme kutoka huko tumeuvusha tumeupeleka ng’ambo ya pili. Na hayo ndiyo makubaliano kwa vitu ambavyo viko upande wa pili, kama upande wa pili hakuna tunafanya kwa pamoja. Na hatuulizani mnapeleka wapi. Tunasema tunapeleka kwa ndugu zake."
}