GET /api/v0.1/hansard/entries/588090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588090/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Lakini tunashughulika sasa na mradi mkubwa zaidi. Kwa bahati nzuri, Tanzania tunavyianza vyanzo vingi vya nishati ya umeme, tumefanya mazungumzo na Rais Uhuru kwamba tuone namna ya kuwezesha Kenya kupata megawati 1000 kutoka Tanzania. Tunachoanza nacho sasa hivi ni kujenga transmission line ya 400KV kwa sababu laini ya 400KV ndio inauwezo wa kusafirisha umeme mkubwa. Makubaliano yameshatiwa sahihi na pia mradi huu tunaweza kupata umeme kutoka Zambia kwa sababu ni Zambia-Tanzania-Kenya interconnect. Ujenzi unaanza upande wetu na tutakuja kuunganisha Namanga. Tumeshaleta bomba la gesi na limeshafika Dar es Salaam. Mradi huu unauwezo wa kuzalisha megawati 3000. Tumesema kwa sasa kwa kuanzia tutatenga megawati 1000 kwa ajili ya Kenya. Interconnect ikikamilika itakua rahisi."
}