GET /api/v0.1/hansard/entries/588098/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 588098,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588098/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tunashindania nini? Mpaka sasa tulichokifanya kidogo ni kama ncha tu ya ukucha.Sasa mmeshafika kwenye ncha ya ukucha ndiyo mnashindana? Mtabaki hapo hapo! Kumbe mna uwezo wa kufanya mpaka ikawa mkono wote. Kwa nini sisi tunasema Kenya ni mshirika wa kimkakati? Katika zile nchi 10 zenye uwekezaji mkubwa Tanzania, Kenya ni ya tano: Ni Uingereza, Uchina, Marekani, India halafu Kenya inafuata. Lakini unapochukua wawekezaji kutoka Afrika, katika wale kumi bora, ziko nchi mbili tu za Afrika – Kenya na Afrika Kusini. Kenya ndiyo inaongoza na Afrika Kusini inafuata."
}