GET /api/v0.1/hansard/entries/588107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 588107,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588107/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "The President of the United Republic of Tanzania",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ", katika uwekezaji kutoka Kenya, asilimia 45 wako kwenye viwanda, asilimia 13 kwenye utalii na asilimia 12 wako kwenye real estate . Kwa hivyo, fursa pale ni nyingi za kuwekeza. Mazingira ya uwekezaji pia ni mazuri na yanawezesha. Lakini waambieni pia uwekezaji uko salama pale. Siku hizi hatutaifishi tena, tumeacha. Lakini pia anayewekeza anaruhusiwa kuchukua faida. Anaweza kuondoka na gawiwo la hisa. Sisi Tanzania ni waumini wa utangamano wa kikanda. Kwetu sisi ni sera na ni jambo la msingi. Tumekuwa waumini wa Umoja wa Afrika. Ndiyo maana Tanganyika na Zanzibar zikaungana kuzaa Tanzania baada ya shirikisho kuchelewa kidogo. Lakini pia ndiyo maana tuko kwenye East Africa Economic and Political Integration na tunaamini kwamba kama nchi za Afrika Mashariki hazitakuja pamoja, uwezo wetu wa kushindana katika masoko hata ya kanda zaidi ya Afrika Mashariki au kwenye dunia utakuwa mdogo sana. Kwa hivyo, sisi wakati wote tutaunga mkono agenda ya utengamano wa Afrika Mashariki na tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba agenda hiyo inatekelezwa kama vile tulivyokubaliana. Katika mazungumzo na Rais Uhuru na viongozi wengine wa Kenya, moyo wa Kenya ni huo huo: kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki ndiyo chombo chetu na sote tukisaidia kiweze kustawi na kufanikiwa."
}