GET /api/v0.1/hansard/entries/588627/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588627,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588627/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Shukrani sana, Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Kwenye Mswada huu, kuna baadhi ya vipengele ambavyo ni lazima nivisisitize. Katika Kifungu cha 34, inaonekana kwamba lugha ambazo zitatumika katika Mahakama Kuu ni Kiingereza na Kiswahili. Mambo haya pia bila shaka yatakuwa na changamoto zake. Moja ya changamoto hizo ni kwamba miongoni mwa wale watakaotumia mahakama hizo, haswa majaji wetu, kutakuwa na umuhimu wa kuhakikisha kwamba wanapata mafunzo mwafaka ya lugha yetu ya Kiswahili. Ijapo Kiswahili ni lugha kongwe, mara kwa mara mambo hugeuka. Ili kesi ziweze kusikizwa na kutatuliwa vizuri katika mahakama zetu, kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba maafisa watakaotekeleza majukumu hayo watapata mafunzo mara kwa mara."
}