GET /api/v0.1/hansard/entries/588628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 588628,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588628/?format=api",
"text_counter": 79,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Mhe. Spika ni wazi kwamba katika kila kaunti ya Kenya, kuna umuhimu wa kuwekwa mahakama. Hii itasaidia wengi haswa waliokuwa wanaenda safari za mbali kutafuta haki. Ikiwa mambo haya yatakuwa, na ninaamini yatakuwa kwa sababu tayari tumeona yakitendeka, wananchi wetu katika Jamhuri ya Kenya hawatakuwa na matatizo ya kutafuta haki. Jambo lingine ningependa kugusia ni lile ambalo Waheshimiwa wenzangu wamegusia haswa kuhusu utatuzi wa kesi Vile sheria yetu ilivyo na hali ya utatuzi wa kesi katika Kenya, ni kwamba yule ambaye atakuwa ameshinda, ameshinda na yule ambaye amepoteza kesi huwa ashapoteza. Lakini ikiwa kama vile ambavyo kifungu cha 26 kimezungumzia, kwamba kutakuwa na nafasi ya mahakama kuleta mawiano ambapo watu watakaa chini na wazungumze ili waweze kutatua kesi, ni mambo ambayo yatasaidia wengi haswa wale wenye matatizo. Kifungu cha 26(3), kimezungumzia utumiaji mbinu ambazo ni za kitamaduni kutatua mizozo. Tunajua wazi kwamba katika Jamhuri yetu ya Kenya katika mahali ambapo watu wanaishi, kuna baadhi ya mambo yanaenda kulingana na tamaduni za mahali hapo. Itabidi watu kukaa chini na kuona wale wataalam katika hali hizi wataweza kushughulishwa vipi katika masuala haya ndiyo mizozo iweze kutatuliwa. Hili ni jambo muhimu kwa sababu mara nyingi utaona kwamba kesi zinafika mahakamani na kuna vipengele fulani ambavyo hutumiwa na unaona labda mtu amepoteza kesi ilhali mtu yule alikuwa na uhakika fulani. Mhe. Spika, jambo lingine ambalo limesumbua hali ya haki katika Jamhuri ya Kenya ni wingi wa kesi. Mara nyingi unapata watu wanaenda mahakamani wakitafuta haki lakini kesi zinazidi kuahirishwa mara kwa mara kwa sababu ya ukosefu wa majaji au sababu zingine. Ikiwa leo hii sheria yetu ambayo tuko nayo tunazungumzia kuhusu majaji kama 200, na wasaidizi wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}