GET /api/v0.1/hansard/entries/588672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588672,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588672/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu wa Mahakama Kuu. Mwanzo, nataka kusema kwamba naunga mkono Mswada huu. Nafurahi kuwa Mswada huu umeweza kuja hapa Bungeni hususan kwa sababu napenda sana kutetea haki za wanyonge. Wakenya wengi wako katika hali hiyo. Pia, Wakenya wengi hawana njia ya kupata haki katika nchi hii. Wananchi wengi sana huteseka sana kwa kukosa haki hapa nchini. Kitu cha kwanza ambacho ningetaka kuangazia ni kwamba Mswada huu unaongeza idadi ya mahakama kuu humu nchini. Hivi sasa, mahakama kuu nchini ni 20 pekee. Zikiongezeka, huenda kila kaunti itapata mahakama kuu moja au zaidi kutegemea ukubwa wake. Mhe. Naibu Spika, sheria hii, kama nilivyosema, itapeleka haki karibu na mwananchi. Mara nyingi, walala hoi huwa wanashindwa kwenda katika mahakama kwa sababu ya ukosefu wa pesa za usafiri wa mara kwa mara. Kwa hivyo, mabwenyenye ama wenye kudhulumu watu wengine ama wenye pesa ndio wana nguvu za kwenda mahakamani. Wakenya wengi hukosa kupata haki katika mahakama kuu za humu nchini. Kwa hivyo, hili ni jambo ambalo limenifurahisha. Jambo lingine ni kwamba, kutokana na kuongezeka kwa mahakama, itabidi tuongeze bajeti za mahaka humu nchini ili tuweze kujenga mahama kuu nyingine ili wananchi waweze kufaidika kama sheria hii inavyosema. Licha ya maswala tofauti ya kisiasa, nawaomba Wabunge wenzangu kuwa wakati wa kutayarisha Bajeti, tusaidiane ili senti ziweze kupatikana ili mahama nyingi yaweze kujengwa ndio Wakenya wengi waweze kufaidika, hususan walala hoi. Mhe. Naibu Spika, watu wengi huteseka kutokana na masuala kama ubakaji wa watoto wadogo na wanawake na kudhulumiwa kwa wanawake mabwana zao wanapofariki. Mara nyingi, watoto mayatima hunyang’anywa urithi wao, na kadhalika. Kwa hivyo, hili ni jambo la busara. Jambo lingine ni kwamba, mwananchi ataweza kupeleka kesi yake katika mahakama kuu na akishindwa, anaweza kukata rufaa hapo hapo – si lazima asafiri kwingineko. Mimi nimeleta Miswada mingi hapa Bungeni kuhusu watoto wa Kiislamu waliodhulumiwa katika baadhi ya shule za upili za umma humu nchini. Kwa mfano, hivi sasa, kuna kesi katika Kaunti ya Isiolo lakini kukata rufaa imebidi kesi hiyo ipelekwe Kaunti ya Meru. Hii inamaanisha kwamba ni lazima mashahidi wasafiri na walale mahotelini. Kwa hivyo, sheria hii itawasaidia mwananchi. Mhe. Naibu Spika, kuongezeka kwa mahakama kuu kutafupisha muda wa kusikilizwa kwa kesi na mahakama. Kuna kesi ambazo zimekuwa mahakamani kwa miaka kumi ama zaidi. Katika hali ilivyo sasa, mmemfanya mwananchi mlala hoi kutumia pesa nyingi – pesa ambazo hana – kufuatilia kesi hiyo. Kwa hivyo, wanaoshinda kesi mara nyingi ni wale watu ambao wana pesa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}