GET /api/v0.1/hansard/entries/588673/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 588673,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588673/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Kifungu cha 26 kinazungumzia mbinu zingine za kutatua mizozo. Kwa kweli, hili ni jambo nzuri sana - ni jambo nzuri kuliko yale ambayo nimeshayazungumzia. Kupitia mbinu hiyo, mwananchi anapokuwa na kesi, hatohitaji kuwa na wakili. Kama tunavyojua, mawakili huitisha pesa nyingi sana kuanzisha kesi yoyote. Mara nyingi, inabidi mtu alipe angalau Ksh50,000 kuanzisha kesi. Mwananchi wa kawaida hawezi kuwa na hela hizo. Kwa hivyo, kifungu hiki kinachozungumzia mbinu hiyo kitamuwezesha mwananchi kwenda kujiwakilisha mwenyewe mbele ya mpatanishi ili aweze kueleza kesi yake. Kesi yake iweze kusikilizwa bila yeye kutumia pesa nyingi kuajiri wakili. Mhe. Naibu Spika, sheria hii itaongeza nafasi za kazi katika Mahakama Kuu. Wazazi waliuza ardhi na rasilmali nyingine za familia zao na kuwaelimisha vijana wao katika vyuo vikuu. Nafasi za kazi zitakapopatikana, vijana hao watapata ajira. Hivi sasa, wengi wa vijana ambao wamehitimu katika vyuo vikuu hawana kazi. Vijana hao wanaishia kufanya kazi ya kusukuma mikokoteni na kazi nyingine ndogo ndogo. Baadhi yetu wanaweza kusema kwamba kama nchi, hatuwezi kulipa wafanyikazi zaidi kwa sababu gharama ya ajira katika sekta ya umma iko juu lakini tukiwa na wafanyikazi wengi, na ikiwa haki itapatikana kwa wepesi na kwa haraka, tutaweza kuokoa fedha nyingi zinazopotea kutokana na kucheleweshwa kwa utendaji haki na mahakama zetu – hali ambayo inaumiza uchumi wetu. Kwa hivyo, badala ya kuendelea kupoteza pesa kupitia hali hiyo, nchi yetu itaokoa pesa. Mwisho, ningependa kuwahimiza wale ambao watakuwa wanawaajiri mahakimu wakuu wahakikishe kwamba watu kutoka makabila tofauti humu nchini wameajiriwa pale nafasi za ajira zitakapotokea. Hususan, wananchi katika eneo la Pwani, ambako nimetoka, wanaona kwamba wanatengwa katika masuala ya kitaifa. Mara nyingi, tunasingiziwa kwamba hatujasoma. Lakini ningependa kulihakikishia Bunge hili kwamba vijana wengi katika eneo la Pwani, hususan katika Kaunti ya Kwale, sasa wamesoma. Wazazi wamejizatiti kuwaelimisha vijana wao. Kwa hivyo, kuna vijana wa kutosha nchini kote waliohitimu kutoka vyuo vikuu. Vijana hao wanafaa kuajiriwa nafasi za kazi zitakapopatikana. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu."
}