GET /api/v0.1/hansard/entries/590321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590321,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590321/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Nimesimama kuunga mkono Mswada huu kuhusu Mahakama ya Madai Madogo ambao umeletwa Bungeni. Kwa haraka, nataka kuwajulisha wenzangu na wananchi kuwa haya mahakama ambayo yatatengenezwa baada ya hii sheria si ya jinai au uhalifu bali ni ya mashtaka kati ya watu binafsi. Kwa hivyo, wasifikirie kuwa ni polisi watakuwa wakipeleka mashitaka katika hayo mahakama. Pili, ni sheria nzuri ambayo inatungwa. Hii ni kwa sababu kwa mara ya kwanza tangu Katiba ipitishwe tuzipa Mahakama za Juu nafasi ya wiki mbili na nyingine miezi sita ili kupeana hukumu wakipelekewa madai ya kuhusu uchaguzi ambao umekumbwa na shida. Kwa mara ya kwanza, Mahakama ya Madai Madogo itakuwa na nafasi ya kuamua kesi kwa siku tatu. Hii ni sheria nzuri kabisa. Lingine wananchi wanastahili kujua kuhusu hii sheria ni kuwa mahakama hizi zitakuwa katika kila kaunti na zinahusu kesi ndogo ndogo au madai madogo madogo ambayo hayazidi Ksh100, 000. Kwa hivyo, kama kesi inazidi Ksh100, 000 inabidi mlalamishi aende katika mahakama za kawaida. Lingine muhimu ni hilo la kuwa hakuna wanasheria wanahusishwa hapa. Mimi ni mwanasheria lakini ukweli ni kuwa watu wengi huko nje hutisha wenzao. Ukienda kupeleka madai yako ambayo ni halali kabisa, mtu hukutisha kuwa ataajiri wakili na wewe utaona. Hii sheria inasema hakuna mawakili. Watu watakuwa wanatoshana nguvu wakienda mbele ya muamuzi atakayekuwa katika hii sheria. Sheria hii imesema Msajili awe wakili. Nakataa hilo. Ni muhimu tubadilishe sheria hii katika sehemu ya tatu ya upitishaji sheria na tuondoe hili pendekezo kuwa Msajili sharti awe wakili. Mtu yeyote aliye na uwezo wa kusimamia ofisi awe Msajili katika mahakama hii. Hamna haja ya kusema tunapunguza uanasheria mwingi halafu tunaajiri mawakili katika kila sehemu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, hili jambo la lugha pia ni zuri sana. Kwa mara ya kwanza, wananchi wataruhusiwa kuongea lugha ya mama ambayo mtu anajisikia anaweza kuelezea madai yake. Hii ni badala ya lazima ya kuwepo na mtu wa kutafsiri kila wakati na kila wakati kuulizwa uongee Kiingereza au Kiswahili. Hii sheria itakuruhusu uongee ile lugha ambayo unajisikia uko nyumbani nayo. Kipengele cha 32 kinasema zile sheria ambazo kwa kawaida zinatumika wakati wa kutoa ushahidi zilegezwe. Unaweza kutoa ushahidi hata kwa simu na mahakama inawezatumia karatasi tu. Ile sheria inayokataza watu na kuwaambia “usiseme hivi, sema vile” imeondolewa hapa. Haya ni mahakama ambayo inawaruhusu watu ambao hawana mawakili, hawana masomo waweze kutoa ushahidi wao haraka haraka. Kipengele ambacho labda nina shaka nacho ni cha 47 ambacho kinasema eti “mtu akipatikana kuwa anastahili kulipa mwingine,” usipolipa unawekwa ndani miezi sita. Hiyo ni sheria mbaya kwa sababu haisemi “kama una uwezo wa kulipa na ukatae ndipo unaweza wekwa ndani.” Kwa kweli imesema ukishindwa kulipa uwekwe ndani. Hiyo ni sheria mbovu kabisa na lazima tuibadilishe na kusema hatua itachukuliwa mtu ambaye ana uwezo wa kulipa lakini anakataa kulipa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}