GET /api/v0.1/hansard/entries/590322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590322,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590322/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Kipengele cha 48 kinasema kuwa mtu anawezapeleka madai yake madogo kwa mahakama nyingine wakati wowote. Nasema hivi: Haina haja tutengeneze haya mahakama halafu turuhusu watu wapeleke madai haya madogo madogo kwa mahakama zingine. Wacha madai ambayo hayajazidi Kshs100, 000 tuyapeleke katika haya mahakama. Sheria hii pia ina shida kidogo. Inasema madai yanayohusiana na kampuni hayawezi kupelekwa katika haya mahakama. Kama madai ni madogo madogo na ni ya chini ya Kshs100, 000, kwa nini tusiseme kampuni ambazo zimeenda mashinani kwa sababu ya kandarasi, pesa zinazokuja kwa kaunti na kadhalika zisipeleke madai na mashtaka yao katika haya mahakama? Hicho ni kipengele ambacho tunastahili kubadilisha. Naunga mkono."
}