GET /api/v0.1/hansard/entries/590626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590626/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wetangula",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 210,
        "legal_name": "Moses Masika Wetangula",
        "slug": "moses-wetangula"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ukisoma historia ya lugha yoyote, hakuna lugha inayowekwa kwa nyungu na kufungwa. Lugha inakuwa kwa kuchanganya maneno kutoka lugha zingine na kujaza.Rais Kikwete huhutubia vikao vya Umoja wa Afrika kwa Lugha ya Kiswahili peke yake. Lugha rasmi za Umoja wa Afrika ni Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania, Kiarabu na Kiswahili. Bw. Spika wa Muda, katika Hotuba yake mojawapo ya vitu ambavyo alitambua ni kwamba nchi anayoongoza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazingatia Umoja wa Afrika Mashariki. Akasema kwamba yeye na wale watakaomrithi wataendelea kuzingatia Umoja wa Afrika Mashariki. Hilo ni jambo muhimu sana kwa sababu nchi ya Kenya imenufaika kibiashara na kikazi kuliko nchi zingine zozote kutokana na Umoja wa Afrika Mashariki. Wakenya ndio wananawiri kila mahali. Ukienda Rwanda, Burundi, Uganda na Tanzania, ni Wakenya ambao wanafanya kazi huko. Kenya imepakana na nchi kubwa kuliko zote Afrika Mashariki. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi pamoja katika hali ya kijiografia. Rais wa nchi hiyo akisema anaunga mkono kikamilifu Umoja wa Afrika Mashariki ni jambo ambalo lazima tusifu. Jambo la pili ni kwamba Rais Kikwete alisema sasa Kenya na Tanzania zimeanza kujenga miundo mbinu ambayo inaunganisha nchi zetu. Barabara ya Athi River- Namanga-Arusha ambayo waliokuwa Mawaziri wa Afrika Mashariki na hata Sen. (Dr.) Khalwale wameitumia mara nyingi, sasa ni barabara nzuri sana. Barabara hiyo ilijengwa na mkopo kutoka Japan. Tanzania walimaliza sehemu yao kwanza. Kenya, katika mbinu zake za kawaida za ufisadi, wakachelewa; sasa wanajaribu kumaliza barabara hiyo katika mji wa Namanga. Barabara ya Arusha-Moshi-Mwatate-Voi haitarahisisha tu uchukuzi kutoka Arusha hadi Voi, lakini pia itapanua biashara kwa wakaazi wa Arusha, Moshi na maeneo ya Kilimanjaro kutumia Bandari ya Mombasa. Hiyo ni biashara na manufaa kwa nchi zote mbili. Tatu, barabara kutoka Dar es Salaam-Tanga-Lungalunga-Diani-Mombasa, pia inafungua njia kubwa ya kuleta biashara kati ya miji ya Dar-es-Salaam na Mombasa. Bw. Spika wa Muda, Rais Kikwete pia alitaja kuuzwa kwa nishati kutoka Tanzania kuingia Kenya na Kenya kuingia Tanzania. Alitaja mji wa Sirare ambako unatoka, Namanga na Monduli. Hiyo ndio njia ambayo tunataka kuona tukiendesha uhusiano wetu jinsi ambavyo tumefanya na Ethiopia. Ethiopia wanatuuzia nishati katika mji wa Moyale ambao haukuwa na stima. Rais Kikwete pia alitaja mambo muhimu ya Katiba. Umeona jinsi mambo yanavyoenda katika kanda hii? Rais wa Uganda amekataa kuondoka ofisini kinyume na Katiba naye Rais wa Rwanda anajaribu kwenda njia hiyo. Rais Kikwete alituambia Bungeni kwamba yeye siku zake zinayoyoma, kura zitapigwa tarehe 25 Septemba, 2015 – mimi ni mmoja wa wale ambao tutaenda kuangalia jinsi kura zinavyopigwa – na baada The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}