HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590628,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590628/?format=api",
"text_counter": 291,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ya hapo, ataondoka ofisini. Hana ulafi, haja wala nia ya kuongeza siku zake ofisini na hata siku moja. Hiyo ni kuheshimu Katiba ya nchi. Hata katika hotuba yake alisema, “Kulingana na Katiba ya nchi yetu, muda wangu umekwisha. Mimi naenda kukaa kama mmoja wa wananchi mashuhuri wa Tanzania nikifuata Marais Mwinyi na Mkapa waliostaafu.” Hilo ni jambo la kusifu sana. Bw. Spika wa Muda, Rais Kikwete ni Rais wa nchi ambayo, mbali na mwaka wa 1977 ambapo Kenya ililumbana na Tanzania walipovunja Muungano wa Afrika Mashariki wakafunga mpaka, Kenya na Tanzania hazijawahi kugombana tena kwa vyovyote vile kwa mambo ya mipaka, biashara na kadhalika. Hadi wa leo, Tanzania sasa ndio imenawiri kibiashara kuliko Kenya katika ununuzi na uuzaji wa bidhaa kutoka hizi nchi mbili. Lazima, pia, tumshukuru Rais Kikwete kwa aliyochangia wakati Kenya ilikuwa katika maafa ya baada ya kura mwaka 2007/2008. Alikuja kama jirani mwema na rafiki, akatusaidia kuleta mapatano na kuunda Serikali ya mseto kati ya Mzee Kibaki na aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga. Kuja kwake kulisaidia kuleta uwiano katika nchi yetu ambao ulisaidia kuleta mapatano ili Wakenya wajue kwamba lazima waishi kama Wakenya na mandugu na waache kulumbana kwa sababu ya kutokubaliana kisiasa. Alichangia pakubwa katika kuisaidia nchi yetu. Bw. Spika wa Muda, mimi naunga mkono yale ambayo Rais Kikwete alisema, kwamba Kenya na Tanzania ni nchi jirani na marafiki wa muda mrefu. Akazidi kusema kwamba ni lazima tushirikiane na nchi zingine za Afrika Mashariki ili kuendesha siasa na uchumi wa kusaidia watu wa kanda hii. Ukiangalia Southern African DevelopmentCommunity (SADC), Economic Community of West African States (ECOWAS), EconomicCommunity of Central African States (ECCAS), ni East African Community ambayo imeendesha mambo yake kikamilifu hadi kufikia upeo wa kuwa na Bunge na Mahakama. Sasa tunakaribia kuwa na uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, badala ya kuchaguliwa na Bunge za nchi wanachama. Hiyo itasaidia kuleta pamoja wananchi wa Afrika Mashariki. Pia, mwananchi wa kawaida huko kwako Sirare, Laikipia au Pokot atajua anapigia kura Mbunge ambaye atamwakilisha katika Bunge la Afrika Mashariki. Huku ndiko kukuza umoja wetu ambao ni wa umuhimu mkubwa. Tunayo ndoto kwamba hivi karibuni katika Muungano wa Afrika Mashariki, sheria itaruhusu Wakenya, Watanzania, Warundi, Warwanda na Waganda kuishi na kufanya kazi popote wanapotaka na hata kutembeleana na kuishi kama ndugu. Hiyo itasaidia nchi zetu kukua kama vile Umoja wa Ulaya umesaidia nchi za Ulaya na kupunguza migogoro na vita na kuleta manufaa kwa wananchi wao. Tunataka kuona Kenya ikifuata utaratibu wa Tanzania wa kupunguza ukabila. Ingawa Rais Kikwete hakuzungumzia swala la ukabila, wewe ni jirani wa Tanzania na unajua kwamba huko, unaweza tu kuuliza Mtanzania jimbo analotoka lakini sio kabila lake. Watanzania wamekumbatia umoja wa nchi yao. Mpaka leo, ukienda Tanzania, ukitoka Kilimanjaro mpaka Mbeya mpaka Mtawala mpaka Songosongo, Mtanzania ni Mtanzania. Hapa Kenya, Bw. Spika, Jumamosi iliyopita ulisoma kwa gazeti kwamba wanateua wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za Serikali. Kati ya 350, 97 wanatoka kabila moja, 65 wanatoka kabila lingine, 77 wanatoka kabila lingine halafu kabila kama ya Sen (Dr.) Khalwale na ya Sen. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}