GET /api/v0.1/hansard/entries/590630/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590630,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590630/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Wako, kati 350, watu saba. Kabila kama la Sen. Orengo, watu 9. Tunajenga nchi gani kama makabila mawili ama matatu yanafikiri Kenya ni himaya yao; Kenya ni nchi yao, wanafanya yale wanataka? Hata wazee wa zamani kama ndugu yangu Sen. G.G Kariuki, wakati wao hawakufanya mambo hivi. Walikuwa wakiangalia nchi nzima. Kama kuna uwezo wa kuwapa wananchi kazi, tungetaka wananchi wote wapewe kazi bila kuzingatia misingi ya kikabila. Hata Elmolo, kabila ndogo kuliko zote, hata Wakuria, kabila ndogo, wana wasomi, maprofesa, madaktari, waandishi na hata mawakili na wanaweza kutoa watu wa kufanya kazi kwa Serikali. Hilo ndilo swala lazima Kenya iige na isome kutoka Tanzania. Tusipofanya hivyo, Bw. Spika wa Muda, tutaendelea kucheza karata na maisha ya wananchi kwa misingi ya kikabila. Leo hapa nchini Kenya, ikiwa hutoki kabila la Rais au Naibu wake, huna lolote Kenya hii. Wanawapatia watu vitu vidogo vidogo wakisema sasa wako Jubilee. Tazama Jubilee ilivyo; ni Rais na mdogo wake. Wamegawana mara mbili na mabaki inaangukia wale wengine wadogo wadogo wanachukulia kutoka chini ya meza, mambo yanaendelea kuharibu nchi yetu. Bw Spika wa Muda, hili ni swala lazima Kenya isome, iige na ifuate mfano wa Tanzania ambayo imeongozwa tangu Uhuru na marais Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Mungu akitujalia, tunaenda kuwa na Rais Magufuli ambaye nafikiri na sina shaka ataongoza nchi hiyo kwa njia ambayo misingi yake imewekwa na wale waliotangulia. Kwa hayo mengi, naunga mkono Hoja hii, na wale waliokuwa na taswishi, sasa wajue kwamba katika Bunge hili, Sen. Boy Juma Boy, wewe, Bw. Spika wa Muda, Sen. Muthama na wengine wachache tunaongea lugha sanifu inayoeleweka na inayotoa yale tungependa kusema bila wasiwasi."
}