GET /api/v0.1/hansard/entries/590632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590632,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590632/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Khalwale",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 170,
"legal_name": "Bonny Khalwale",
"slug": "bonny-khalwale"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii ambayo inahusu Hotuba ya Rais wa Tanzania alitutolea sisi kama viongozi wa Bunge la Seneti na wale wa Bunge la Kitaifa. Furaha yangu ni kwamba wakati Rais wa Tanzania alipokuwa akitoa Hotuba yake, Wakenya wote walikuwa wakisikia hiyo habari. Ilikuwa funzo kubwa kwa wale wanaochochea demokrasia kusikia Rais akisema amekubaliana na maagizo yaliyoko. Katiba ya Tanzania haimrusu kuwa rais zaidi ya miaka kumi. Ninamshukuru Rais Kikwete na ningependa hii iwe funzo sio tu kwa Wakenya bali kwa Waafrika kwa jumla. Bw. Spika wa Muda, mtu kuwa rais ni nafasi kubwa ambayo marais wa Afrika wametumia kupora mali ya umma. Viongozi, na sitazungumzia hao viongozi---"
}