GET /api/v0.1/hansard/entries/590637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590637,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590637/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "hii iwe funzo kwa wananchi wa Congo, kwa sababu Congo, Rwanda na Burundi wako katika harakati ya kujaribu kubadilisha katiba zao ili wawapatie marais wao nafasi ya kuendelea kuwa uongozini. Hii sio njia ambayo sisi kama viongozi wa Afrika tungependa yawe mambo ambayo kila nchi itatumia. Bw. Spika wa Muda, maoni yangu ya pili nikiunga mkono hii Hotuba yanahusu matamshi ya Rais Kikwete kwamba yeye anajivunia ule uhusiano mwema ulioko kati ya Kenya na Tanzania. Ningependa kumuunga mkono kwa sababu mambo ya biashara tusipoyatilia mkazo kati yetu na nchi jirani, hatuwezi kufaidika na wingi wa watu walio katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Unakumbuka ulipokuwa Waziri na mimi nikawa naibu wako, tulifanya kazi nzuri sana kule Arusha. Nakumbuka ulituongoza mpaka wakati huo tukatolewa tukiwa tumefanya hali ya biashara ikiwa imeanza kunawiri sana kati ya Tanzania na Uganda. Bw. Spika wa Muda, nikizungumzia huu uhusiano, ningependa kupongeza nchi za Tanzania na Kenya kwa sababu katika Jumuiya, ni sisi wawili pekee tunaozingatia demokrasia ya kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Mheshimiwa Rais wa Tanzania, niliskia kama ana wasiwasi kidogo, eti pengine chama chake cha kisiasa; Chama Cha Mapinduzi (CCM), kisiposhinda, alihofia kwamba pengine uhusiano wetu utaharibika. Mimi nina hakika kwamba hata yule mpinzani wao, Mheshimiwa Lowasa, ambaye ni rafiki yangu; tulikutana kule Arusha, ni Mwafrika ambaye anaamini kwamba Kenya ni muhimu kwa Watanzania. Sisi hatuwezi kutishwa, wale tunaompenda Lowasa, hivi karibuni tutaenda Arusha na kumpigia debe ndio apate nafasi ya kushinda kura. Kuhusu uhusiano wa nchi hii na Tanzania, Rais alitaja mambo ya michezo. Lazima Wakenya wakumbuke kwamba kuna vijana wetu wengi wanaocheza kandanda kule Tanzania na kuna wale kutoka Tanzania wanaocheza hapa, hata mchezo wa ndondi, kuna wale wanacheza hapa Kenya wanaotoka Tanzania. Kwa hivyo, mimi ningependa kumuunga mkono kwa jambo hilo. Bw. Spika wa Muda, Rais alikumbuka kwamba mwaka wa 2007/2008, alikuja hapa kutusaidia tulipokuwa tukipigana kwa ajili ya matokeo ya uchaguzi wetu. Ningependa kuwahimiza wanachama wa Jubilee kuyatilia maanani matamshi ya Rais Kikwete kwa sababu naona mzaha umeanza. Viongozi wa Chama ya Jubilee wanazunguka nchi nzima wakifanya maombi ya kitaifa. Kutokana na maombi hayo, nchi imeanza kugawanyika. Wanasiasa wa Jubilee wanatamka maneno yasiyo na msingi kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu ndiye aliyempendekeza Naibu wa Rais apelekwe International Criminal Court (ICC). Huo ni uwongo kwa sababu wakati wa vita vya Post Election Violence (PEV), Naibu wa Rais na aliyekuwa Waziri Mkuu walikuwa katika chama kimoja. Viongozi waliojiunga na siasa hivi majuzi na wasiojua historia kama hii, wanafaa kukimya kabisa. Bw. Spika wa Muda, kile Naibu wa Rais anahitaji hivi sasa si maombi, bali mawakili hodari watakaomsaidia katika kesi yake katika Mahakama ya Jinai kule The Hague."
}