GET /api/v0.1/hansard/entries/590641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590641,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590641/?format=api",
    "text_counter": 304,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Walioathiriwa na vita hivyo ni watu kama wewe, Rais Moi na mimi. Gari langu lilichomwa na biashara yako ikavamiwa. Boma yake Rais mstaafu Moi ilibomolewa ingawa hatukuhusika na vita hivyo vya PEV. Sisi ndio tulihisi uchungu wa vita hivyo. Tunataka Kenya iwe na amani. Bw. Spika wa Muda, Rais Kikwete alizungumzia Barabara ya Athi River- Namanga-Arusha. Alituarifu pia wamekubaliana na Rais Uhuru kutengeneza barabara ya Taveta-Holili-Moshi-Arusha. Hata hivyo, lilikuwa jambo la kusikitisha Rais Kiwete aliposema kwamba ujenzi wa barabara huo umezinduliwa upande wa Kenya pekee. Ikiwa tutangeneza upande wa Kenya pekee basi tutakuwa tumepoteza pesa zetu kwani hakuna mwanabiashara atakaye peleka lori lake katika barabara hiyo ikiwa atasafiri vyema kutoka Taveta hadi Holili kisha apate barabara mbovu afikapo hapo. Hivyo, namhimiza Rais wa Tanzania kuzingatia ukarabati wa barabara ya Taveta-Holili-Moshi-Arusha ili ujenzi uanze mara moja. Mwisho, ninamshukuru Rais Kikwete kwa kuzungumzia jambo la uekezaji. Alisema wako tayari kuwapa Wakenya nafasi zaidi za kuekeza katika Tanzania. Mimi kama mojawapo wa waliowahi kufanya kazi Tanzania, tuna nafasi nyingi za kuekeza katika biashara za hospitali na shule za kibinafsi katika Tanzania. Naomba kuunga mkono Hoja hii."
}