GET /api/v0.1/hansard/entries/590645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590645,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590645/?format=api",
    "text_counter": 308,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Prof.) Lesan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 506,
        "legal_name": "Wilfred Rottich Lesan",
        "slug": "wilfred-rottich-lesan"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kumshukuru Rais wa Tanzania kwa ziara aliyofanya humu nchini. Pia, namshukuru kwa usaidizi aliyoipa nchi yetu ya Kenya wakati wa PEV mwaka wa 2007/2008. Usaidizi aliotupa hauwezi kulinganishwa na pesa. Pili, naitakia Tanzania mema wakati huo ambao wanajitayarisha kufanya uchaguzi mkuu. Nawaombea wawe na uchaguzi mwema bila tashwishi yoyote ili tuweze kuendelea kufanya kazi pamoja. Rais wa Jamhuri ya Tanzania alizungumzia biashara kati ya Taifa letu la Kenya na Tanzania. Bidhaa za Kenya zinazosafirishwa Tanzania zinagharimu US$ 300 milioni. Tukilinganisha na bidhaa zinazosafirishwa Uganda kutoka Kenya zinagharimu US$7 million. Tanzania ina idadi kubwa ya watu. Kwa hivyo, inatupa soko kubwa ya bidhaa zetu ikilinganishwa na Uganda. Bw. Spika wa Muda, nachukuwa fursa hii kuhimiza nchi za Kenya, Tanzani na Uganda kushirikiana kibiashara ili zinawiri na kufaidi wananchi wa nchi hizi tatu. Pia, ningependa kuwahimiza viongozi wa mataifa ya Afrika Mashariki wawe wakitembeleana wakiwa katika uongozi na kupeana hotuba katika Bunge na kuarifu mataifa yote kuhusu miradi wanayoendeleza. Pia, itakuwa mfano mzuri kwa viongozi wa mataifa ya Afrika Masharaki kuona ya kwamba wanatii sheria za nchi zao. Hivi sasa, kuna mjadala kuhusu kipindi cha uongozi kwamba rais anapaswa kutawala kwa muda wa miaka kumi tu ili demokrasia idumu katika mataifa yetu. Kwa hivyo, nampongeza Rais wa Jamhuri ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}