GET /api/v0.1/hansard/entries/590675/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590675,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590675/?format=api",
"text_counter": 338,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okong’o",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 948,
"legal_name": "Kennedy Mong'are Okong'o",
"slug": "kennedy-mongare-okongo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii nichangie Hoja hii kutokana na Hotuba ya Rais wa nchi jirani ya Tanzania, Mhe. (Dkt.) Jakaya Kikwete, katika Bunge la Kenya. Nampongeza Rais huyo kwa unyenyekevu na uzalendo wake kwa Jumuia ya Afrika Mashariki. Rais Kikwete amefuata nyayo za waliomtangulia; Mwalimu Kambarage Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kwa kuleta utangamano wa Tanzania na mataifa mengine ya Afrika Mashariki. Rais Kikwete alizungumzia maswala ya uwekezaji katika Tanzania. Ningependa kuyatilia mkazo mawazo ya Seneta wa Kaunti ya Kakamega, (Dkt.) Khalwale kwamba Wakenya wana nafasi nzuri ya kuekeza Tanzania katika sekta ya elimu, viwanda na hospitali. Tanzania walipokuwa na mfumo wa ujamaa, walibaki nyuma kwa muda mrefu. Wakati huu, wanafuata mfumo wetu na watapiga hatua ya kimaendeleo. Mwalimu Nyerere aliwaelezea Watanzania kwamba wakitaka kutembea Ulaya, wasiende mbali sana, lakini waje hapa Nairobi. Hata hivyo, Tanzania imeendelezwa kiuchumi sana na viongozi waliokuja baada ya Mwalimu Nyerere. Bw. Spika wa Muda, kuna vizuizi ambavyo vilisababisha kusambaratika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki mwaka wa 1978. Ikiwa tunataka utangamano, lazima wataalamu wanashughulikie maswala yaliyosababisha kutibuka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka wa 1978 ndiposa Jumuia ya Afrika Mashariki iimarike. Rais Kikwete alizunguzia kuhusu kusaidiana katika mambo ya kijasusi na ni muhimu sana lakini ningependa kuhimiza nchi ya Tanzania izingatie maswala ya haki za binadamu ili watu wanaoshikwa nchini humo wasidhulumiwe bila kufuata sheria. Rais Kikwete ambaye hatamu yake ya uongozi imeisha na ingawa hajazeeka, ameamua kung’atuka kisheria. Napendekeza kwamba wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kung’atuka uongozi, naomba kwamba tumpendekeze Mhe. (Dkt.) Kikwete kuchukua cheo hicho. Bw. Spika wa Muda, kumekuwa na tashwishi katika utangamano. Kwa mfano, Kenya, Uganda na Rwanda karibu zitenge Tanzania. Kwa vile Rais alisema kuwa yuko tayari kuimarisha Muungano wa Jumuiya, basi sisi tuna nafasi nzuri katika uwekezaji kwa sababu Watanzania ni ndugu zetu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}