GET /api/v0.1/hansard/entries/590678/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590678,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590678/?format=api",
    "text_counter": 341,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Ninashukuru sana kwa nafasi hii, Bw. Spika wa Muda. Nimesikiza waheshimiwa waliozungumza na walioshindwa kuzungumza Kiswahili. Niligundua kwamba umoja wa taifa hili uko mbali. Hii ni kwa sababu kitu kimoja kinachounganisha watu ni lugha ambayo wanatumia. Tumekuwa tukitumia Kiingereza hadi maeneo ya kata. Utapata mtu anaongea na wananchi kwa dakika tano au kumi kwa lugha ya kigeni. Wananchi wataelewa asilimia mbili tu ya maneno yaliyosemwa. Hawataelewa asilimia 98 ya yaliyosema. Natoa mwito kwamba tukienzi Kiswahili kwa sababu Kiswahili kimeunganisha nchi ya Tanzania. Kiongozi yeyote anayekwenda mashinani hueleweka kila anapozungumza katika mkutano. Ni jambo muhimu kuwa tujifunze na kukikuza Kiswahili ili kituunganishe sisi kama Wakenya. Ni aibu kubwa sana katika taifa letu kwa sababu katika sehemu fulani za nchi yetu, hakuna mtu anayejali kama unaelewa yale wanayosema. Utakuta watu wanazungumza kwa lugha ya mama kuanzia mwanzo hadi mwisho. Bw. Spika wa Muda, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Mhe. Nyerere, alikuza Kiswahili na kuwaunganisha Watanzania. Nakumbuka nikisikiza nyimbo za Shirikisho la Afrika zikiimbwa. Walioleta Shirikisho hilo ni hayati Mzee Jomo Kenyatta, Nyerere na Obote. Wakati huo, tulizungumza kama nchi moja ya Afrika Mashariki. Hata hivyo, juzi tulishuhudia msukosuko uliohusisha Tanzania na Kenya na kusababisha mipaka yetu kufungwa. Haingewezekana Tanzania na Kenya kufikia mahali ziko katika mambo ya biashara wakati mpaka ulikuwa umefungwa. Kwa hivyo, hotuba yaliyotolewa na Mhe. Rais (Dr.) Kikwete ya kutuweka pamoja kama ndugu ni muhimu. Bw. Spika wa Muda, Rais mwenyewe alisema kwamba Wakenya ni nambari mbili kati ya wawekezaji katika nchi ya Tanzania. Sisi ni nambari moja katika Bara la Afrika. Hutasikia Wakenya wanaofanya kazi huko wamehusika katika wizi, rushwa au magendo kwa sababu wanaheshimika sana. Daktari mzuri wa kufanya kazi Marekani anapatikana Kenya; mwalimu mzuri wa kufundisha Rwanda, anapatikana Kenya na dereva mzuri wa kufanya kazi Uganda anapatikana Kenya. Wakiwa huko, hao ndio tegemeo la nchi zao. Lakini ukija hapa kwetu nyumbani unashangaa na maneno kama vile; ‘huyu ni mwizi’, ‘huyu aliiba jana’, ‘usiguze huyu ni wetu’. Tunazuia wizi kwa misingi ya kikabila. Ikiwa jina lako ni ‘Ndung’u’ na umeshukiwa na wizi, unaona Kamau na wenzake nyuma yako. Ikiwa jina lako ni Mutiso ama Onyango, ni vivyo hivyo. Leo, Tanzania wanafanya uchaguzi mkuu. Uchaguzi unaoendelea Tanzania unawahusisha wapinzani Mhe. Magufuli na Mhe. Lowassa. Mhe. Lowassa alikuwa Waziri Mkuu nchini Tanzania lakini kwa kutajwa tu na kudhaniwa, ila si kupatikana, ya kwamba alihusika na magendo, hakupewa tiketi ya uwaniaji na Chama Cha Mapinduzi (CCM) maanake CCM. Hii kwa sababu inazingatia uwazi na utawala wa nidhamu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}