GET /api/v0.1/hansard/entries/590682/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590682,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590682/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mositet",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 608,
        "legal_name": "Peter Korinko Mositet",
        "slug": "peter-korinko-mositet"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda. Hotuba ya Rais wa Tanzania, (Dkt.) Kikwete, ilikuwa nzuri kwa sababu ilikuja wakati ambao anaenda kustaafu. Swala kubwa sana alionyesha ni kwamba anatii Katiba ya nchi yake, anajali maslahi ya wenyeji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na pia ana mapenzi na maono mazuri. Lakini zaidi, alionyesha kwamba hana tamaa ya utawala na anatii Katiba yao. Tuna nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile Burundi, Rwanda na Uganda ambako marais wao wanafanya kila wawezalo kubadilisha Katiba ili waendelee kutawala. Ni vizuri wajue kwamba wakati tu utafika wang’atuke na wengine waingie mamlakani. Bw. Spika wa Muda, kaunti yangu inapakana na nchi ya Tanzania na hata kwa wale ambao wanagombea uongozi kule, sisi tunawatakia kila la heri. Tungetaka Bw. Lowassa ashinde na hata mimi niweze kusema ndugu ya babangu anaishi Tanzania na tunatenganishwa na mipaka ambayo iliwekwa na Wazungu lakini tukienda kule, tuko nyumbani."
}