GET /api/v0.1/hansard/entries/590688/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 590688,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590688/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 431,
        "legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
        "slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
    },
    "content": "Asante sana kwa fursa hii, Bw. Spika wa Muda. Vile ninatamatisha Hoja hili, ningependa kuzungumzia matatu. Historia yetu na Tanzania ikiwemo ile historia ya former Sultan of Zanzibar. Hilo nitalizungumzia siku nyingine. Pili, ni sera ya washiriki wa Afrika Mashariki kujaribu kuitenga Tanzania. Mwisho, ningependa kuzungumza juu ya ile hofu ambayo Rais Kikwete aligusia kuwa Bw. Magufuli akiwa Rais, kwa vile ana uhusiano na ushirikiano na mtu fulani ambaye ni kiongozi katika maswala ya upinzani hapa, huenda Tanzania ikabadilisha sera zao. Hiyo ni hofu ya kitoto. Nakumbuka Rais Kikwete alisema hakuna wajinga kama hao Tanzania. Mimi pia, naomba Kenya tusiwe na wajinga kama hao wa kufikiria mambo madogo kama haya. Watu wako na uhusiano na urafiki kabla, ndani na baada ya siasa. Hiyo haimanishi itabidilisha sera. Sisi kama Wakenya tushirikiane tuhakikishe kwamba tumekumbatia Tanzania kwa sababu tuna mengi yanatuleta pamoja kuliko yale ambayo yanatutenganisha. Nimesikia eti Watanzania ni watu wapole na wakuomba radhi na sisi Wakenya ni mabepari, watu wa nguvu zaidi. Kila mtu ana uzuri na ubaya wake. Sisi tunayaangalia yale mazuri na ule utulivu na utaratibu wa Watanzania. Ni jambo ambalo lazima tulitie ndani ya roho zetu. Huu ubepari wetu umetufikisha wapi sasa? Watu wamefisadi nchi nzima, wakaiba shamba tangu uanzilishi wa taifa hili. Watu waliiba mashamba katika taifa hili wakati wa mwanzilishi wa taifa hili,wanaiba katika kaunti zetu.Waanzilishi wa taifa letu la Kenya ndio matajiri zaidi baada ya vizazi vitatu.Waanzilishi wa kaunti zetu watakuwa zaidi kutokana na wizi wanaouendeleza. Kwa hivyo, tufuate mikakati na msimamao wa Tanzania wa kujua ukweli na usawa katika kuhakikisha kwamba tunaheshimu mali ya wananchi wa taifa hili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}