GET /api/v0.1/hansard/entries/590694/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590694,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590694/?format=api",
"text_counter": 357,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ": Bw. Spika wa Muda, nachukua nafasi hii kuwashukuru wenzangui kwa kuchangia Hoja hii. Kile ambacho kimejitokeza katika Hoja hii leo ni dhihirisho kwamba sisi sote tulifurahia Hotuba ambayo ilitolewa na Rais wa Tanzania, Mhe. (Dkt) Jakaya Mrisho Kikwete. Jambo la pili, sisi kama Wakenya tumefurahi ya kwamba Rais Kikwete anaheshimu Katiba ya Tanzania, na atang’atuka mamlakani wakati wake ukifika. Sisi kama watu wa Bara la Afrika tunasema kwamba huo ni mfano mzuri kwa viongozi wengine. Hata sisi hapa Kenya tumekuwa na mabadiliko katika nyadhifa za uongozi kutoka mmoja hadi mwingine. Ni maombi yangu kuwa siku zijazo tutaendelea na mtindo huu. Tusije tukabadilisha Katiba yetu. Ni lazima tuiheshimu Katiba yetu. Mwisho, ninakubaliana na wenzangu kwamba kulikuwa na shaka kuhusu mstakabali wa uhusiano kati ya Kenya na Tanzania. Rais Kikwete amefanya vyema kuleta ujumbe kwamba anapoondoka mamlakani ana imani na anatarajia kuona uhusiano wa nchi zetu mbili ukimarika zaidi. Pia, ametuhakikisha kwamba kama mzee atafanya kila juhudi kuona kwamba uhusiano baina ya nchi hizi mbili; Tanzania na Kenya, umekuwa bora. Ninawapongeza wenzangu wote kwa kuchangia Hoja hii. Mimi ningependa kuona uhusiano huu wa taifa la Tanzania na Kenya ukiimarika. Bw. Spika wa Muda, nimetimiza jukumu langu. Ninaomba kupendekeza Hoja hii."
}