GET /api/v0.1/hansard/entries/590869/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 590869,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/590869/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia naunga mkono Mswada huu ambao ukipitishwa, utaimarisha mahakama zetu za rufaa. Wakenya wengi wamekuwa wakilia ili kuhakikisha kuwa wamehudumiwa kwenye korti zetu humu nchini, ili masuala yao yashughulikiwe na hukumu kutolewa wakati unaofaa. Mswada huu ukipita, Mahakama ya Rufaa itazunguka nchi nzima. Itakuwa na majaji wasiopungua 12. Itapewa ruhusa na Jaji Mkuu wa Mahaka ya Juu na kutekeleza majukumu yao ili Wakenya wapate huduma hii, ambayo ni ya muhimu. Katibu ambaye atasimamia masuala ya Korti ya Rufaa amepatiwa majukumu ambayo yataiwezesha mahakama hiyo kufanya kazi yake vilivyo, kulingana na Kipengele cha 164 cha Katiba yetu. Wakenya wengi hungojea muda mrefu sana ili kesi zao zisikizwe, na hupata uamuzi wa mahakama baada ya muda mrefu. Kesi nyingine zimechukua miaka isiyopungua mitano na kuendelea. Tangu kuwepo kwa Katiba mpya, Jaji Mkuu amehakikisha kwamba wamepunguza kazi ya kesi ambazo zilikuwa mbele yao. Lakini kwa sababu ya uhaba wa majaji, wameshindwa kutekeleza wajibu wao haraka iwezekanavyo. Mswada huu ukipitishwa, utaiwezesha Mahakama ya Rufaa kuwahudumia Wakenya. Zaidi ya hapo, ni kumrahisishia kazi Jaji Mkuu, ambaye anasimamia upande wa mahakama humu nchini, ili kazi iweze kupunguzwa kwa haraka. Vile vile, majaji wakiwa wengi, wataweza kugawanya kazi kwa urahisi na kusikiza kesi zilizoko ili kuweza kufanya uamuzi kwa muda unaofaa. Suala la majaji kwenda likizoni pia limeangaziwa. Wananchi watafahamu kuwa ikifikia wakati fulani, majaji wa rufaa hawatakuweko kwa sababu watakuwa wameenda likizoni na watu na mawakili wao watajipanga. Wakenya wamekuwa wakiumia sana wakilipa pesa kuwafidia mawakili kwa kazi ambayo wanawafanyia. Wanalipa pesa nyingi kwa sababu kesi zao zinakaa kortini kwa muda mrefu. Mswada huu ukipitishwa, utaiwezesha mahakama kutekelza kazi yake kwa muda unaofaa. Kila mtu Kenya ameshajua faida ya sheria tulizonazo. Kwa hivyo, kila mtu anakimbilia kupeleka malalamishi yake kwenye Korti ya Rufaa. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu uwe sheria ili iweze kuwasaidia Wakenya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}