GET /api/v0.1/hansard/entries/591247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591247,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591247/?format=api",
"text_counter": 313,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Leo nimeamua kuongea lugha ya Kiswahili ili pengine – nasisitiza neno “pengine” - wale wanaohusika wafahamu maneno yangu na hisia za Wakenya kwa jumla. Tarehe 12 Oktoba 2015, katika Chuo Kikuu cha Maseno, wanafunzi walikuwa katika hali ya kufanya siasa zao na kupiga kura. Wanafunzi hao waliingiliwa na wakafukuzwa katika chuo chao. Walitandikwa na hatimaye maisha ya Wakenya watatu yakapotea. Mali ilipotea na wengi zaidi wakapata majeraha. Nataka kuuliza swali ambalo nimeuliza siku nyingine na wengi wameuliza. Swali hili linaenda kwa maafisa wa polisi. Ni maswali matatu."
}