GET /api/v0.1/hansard/entries/591251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591251/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Nataka kutoa mfano mmoja uliotokea katika maeneo ya Mvita. Ni jambo la kusikitisha lakini majambazi - na jambazi hana jina jingine ila “jambazi,” wala muovu hana jina jingine bali “muovu” - walifika na wakampiga risasi askari aliyekuwa analinda benki fulani. Baada ya kumpiga risasi, wakampokonya silaha aina ya G3. Suala ni lile lililotekelezwa na polisi baadaye; likawa ni la kusikitisha zaidi. Nataka kusisitiza kuwa hatuyaungi mkono na tunayakashifu masuala ya bunduki kuwa mikononi mwa majambazi. Lakini, la kusikitisha likawa ni watu takriban 180 kuingiliwa katika mitaa na kushikwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}