GET /api/v0.1/hansard/entries/591252/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 591252,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591252/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Naibu Spika wa Muda, katika watu hao 180, mmoja ni bubu; hawezi kuzungumza wala kusikia na mwingine ana akili punguani. Sasa fikiria askari awezaye kwenda kumtoa mtu mwenye akili punguani nyumbani, kumshika na kumuweka ndani. Vijana wa miaka 14 na 16 wanaofaa kuingia katika shule walikuwa katika mahakama siku ya pili. Sheria ambayo imewashitaki ni kuwa walipatikana wanarandaranda barabarani."
}