GET /api/v0.1/hansard/entries/591412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591412,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591412/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 431,
"legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
"slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
},
"content": "Shukran sana, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Ninafikiri kwa vile jana tulianza na tabia ya kuzungumza Kiswahili kidogo mpaka leo, bado naona ile lugha ya Kiswahili iko katika gia. Mwanzo kabisa ninataka kukushukuru Kamati yako akiwa Naibu wa Mwenyekiti Seneta Mutula Kilonzo Jnr., na mawakili wakubwa katika Seneti hii pamoja na ndugu zetu ambao si mawakili ambao walikaa katika Kamati hii kama vile Sen. Lesuuda, Sen. (Eng.) Muriuki, Sen. Billow, Sen. (Dr.) Khalwale na Sen. Halima Abdille. Hii inaonyesha kwamba huu ni mchanganyiko, kwamba si tu kufuatia hisia za wanasheria na kujifanya kwamba wanasheria ndio wanafahamu kila kitu, lakini ni kuchukua hisia za Wakenya wote kwa ujumla ili tuweze kunufaisha hii harakati yetu. Bw. Spika wa Muda, tulijaribu harakati kama hii miaka miwili iliyopita na kidogo tukafikia ukingoni bila yale madhumuni yetu kuafikiwa. Nafikiria sasa baada ya kukaa katika hili Jumba la Seneti kwa muda mrefu zaidi, tumejua wapi Jumba hili linavuja, na tunaambiwa kuna wakati mtu anafaa kubadilisha katiba na wakati haufai. Lakini mimi ninasema hata kama nyumba ni mpya, kama inavuja lazima uzibe ule ufa ama utaenda kujenga nyumba nzima. Hata kama gari ni jipya latoka DT Dobie, kama breki haifanyi lazima uende ukatengeneze breki ama uende ukapata ajali. Nafikiria hivi ndio tunajaribu kufanya leo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}