GET /api/v0.1/hansard/entries/591414/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 591414,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591414/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, wale ambao walioleta hikii kiungo kinachoitwa Seneti, malengo yao ni kwamba katika mpangilio wowote wa ugatuzi, lazima kuwe na kiungo ambacho kinaweza kulinda ugatuzi. Na sisi hapa tunaambiwa leo kwamba sisi kama Jumba la Seneti, malengo yetu makubwa ni kulinda ugatuzi. Bw. Spika wa Muda, leo wewe ukiambiwa ulinde Benki Kuu ya Taifa huwezi ukapatiwa fimbo kuilinda benki kama hiyo wala ukapatiwa rungu. Kila tukipita katika benki za Kitaifa nyingi tunaona watu wamejiandaa na mabunduki na kadhalika, kwa sababu wanajua wanalinda rasilimali, wanalinda benki kutoka majambazi sugu. Kwa hivyo, sisi leo tumepatiwa tulinde ugatuzi na tumepatiwa fimbo. Tunasema lazima tuongezewe zile silaha za kuweza kulinda ugatuzi kwa namna ambayo ugatuzi utaafikia ile dhamira ya Wakenya wote kwa ujumla. Bw. Spika wa Muda ninashukuru Kamati yako kwa mapendekezo yake. Nimeiona ratiba mliyopendekeza lakini tutibu kidonda hicho haraka iwezekanavyo kabla wakati haujapita sana. Hatuwezi kuendelea katika hali hii ya kutoweza kulinda pesa zinazopelekwa mashinani. Kwa hivyo, ni lazima tufanye haraka iwezekanavyo ili tupate suluhu ya jambo hili. Juzi, nilimskia Rais wa Tanzania akisema kwamba katika nchi yake, hakuna watu wajinga. Tanzania ina umoja. Baada ya miaka kumi, kiongozi anang’atuka uongozini na kumpisha kiongozi mwingine. Aliposema hivyo, nilihisi kwa njia moja au nyingine kwamba anajaribu kusema Kenya ina watu wa aina hiyo. Katiba tuliyonayo ingekuwa inafanya kazi vyema, ingekuwa hatutumii sera za ujinga katika kuendeleza Katiba yetu. Ningependa tuzingatie falsafa ya Abunuasi kwani kiongozi aliyechaguliwa katika eneo Bunge moja, ilhali mimi nilichaguliwa na maeneo Bunge sita, nitakua aje chini yake? Hiyo ni falsafa ya Abunuasi. Ni lazima tupambane nayo kisheria. Hakuna mtu yeyote Kenya mwenye shaka kwamba Seneti ndio Bunge kubwa kuliko Bunge la Kitaifa. Kama kuna yeyote mwenye shaka, lazima tuipindue shaka hiyo kwa njia za kisheria na kikatiba. Nilikubaliana na Kamati hii kwamba tuwe na tume mbili; tume ya Bunge la Seneti na tume ya Bunge la kitaifa kwa vile sisi kama Maseneta hatuwezi kutekeleza majukumu yetu ikiwa hatutapewa uwezo fulani. Hatutaki hazina ya Constituencies Development Fund (CDF) kama wenzetu au Hazina ya Maendeleo ya Kaunti yaani County Development Fund ili kutekeleza majukumu yetu. Bali sisi kama Maseneta tulio na wafanyikazi watatu hivi na askari mmoja, hatuwezi kuyatekeleza majukumu yetu kwa taifa la Kenya. Lazima tupewe ofisi iliyo na uwezo; maafisa wa kufanya utafiti, mawakili na maafisa wa kushughulikia maswala ya bajeti na maafisa wa maswala ya hazina na maadili ya kikatiba. Lazima tutibu janga hilo. Bw. Spika wa Muda, sasa wakati umefika ambao Waswahili husema lazima tuonyeshe ushujaa na ujeuri. Ndugu zetu wa Bunge la Kitaifa wametuonyesha ujeuri mkubwa na wazungu husema nguvu huheshimu nguvu pekee, kwa Kingereza,’ Powerrespects power ’. Hatufai kujidhalilisha mbele ya ndugu zetu wa Bunge la Kitaifa. Lazima tupambane na ujeuri wao. Juzi nilisikia wengine wao wakitoa pendekezo kwamba watachukua Kshs1 bilioni ya hazina ya usawa, ‘ Equalization Fund ’, ije katika milki ya Wabunge na hivyo nasi watupe Kshs1 bilioni waliotunyang’anya katika bajeti ya mwaka huu 2015/2016. Niliwaona wakiwa wepesi wa fikra sana na wenye madharau wakidhania kwamba sisi tunaweza kukigeuza kipengee cha kwanza cha Katiba ya Kenya kwa kutoa neno ‘county’ The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}