GET /api/v0.1/hansard/entries/591418/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591418,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591418/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tukiwa na tume ya kuangalia maswala yetu ya Seneti na nyingine ya kuzingatia maswala ya Bunge la Kitaifa, itakuwa vyema kwani jambo hilo litatuwezesha sisi kuendeleza ratiba zetu. Tumekuwa na nafasi ya kuona vile Bunge la Seneti la Nigeria na United States of America (USA) yanavyoendesha shughuli zao. Nasi pia ikiwa tutalinda ugatuzi hapa Kenya, lazima tugawe majukumu. Majukumu kama kamati teule ya kuchunguza Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Sheria limepewa Bunge la kitaifa. Hilo ni jambo jema. Lakini wale wanahifadhi ya kikatiba, yaani ‘ constitutional tenure ’, kama majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufaa, watachunguzwa na Bunge la Seneti. Bi. Spika wa Muda, tuna ugatuzi katika taifa letu la Kenya lakini kuna watu wenye fikira kwamba Bunge hili la Seneti halina faida. Yeyote mwenye mafikira hayo ni mtu ambaye haelewi misimamo na misingi ya kikatiba na maswala ya ugatuzi. Kile ambacho lazima tujumuike kufanya ni kuhakikisha kwamba tuna uzani na nguvu ya kupitisha sheria zetu bila kupitisha miswada yetu katika Bunge la Kitaifa ili kupata makubaliano. Nakubaliana na mambo yalivyo hivi sasa. Hata hivyo, Seneti lina uwezo mwingi kuliko Bunge la Kitaifa. Itakuwaje sisi tuchaguliwe katika maeneo Bunge mengi na tuwe chini yao? Ndugu yangu, Seneta wa Kakamega alichaguliwa katika maeneo Bunge 12 itakuwaje tuogope kusema kwamba, hili ndilo Bunge la juu? Wengi wetu hapa tuliwapitisha Wabunge wetu na vivyo hivyo tutaenda kuwabwaga kwani wamekosa hisia ya kulinda ugatuzi. Leo tumetiwa hofu eti Wabunge wa Kitaifa watapinga Mswada wetu. Lakini sisi hatuogopi kwani tunataka kupingwa. Wakati tunapingwa ndipo tunapata fikira. Mtu asipopingwa, yeye huzembea. Mtu anapopingwa ndipo anapopata maarifa zaidi. Kwa hivyo, nawahimiza wenzangu hapa wasiogope kupingwa. Wabunge wengine hata katika chama chetu wanaogopa kuwa Mswada wetu utapingwa lakini mimi siogopi kupingwa. Mswada huo ukipingwa na Bunge la kitaifa, utaungwa mkono na Wakenya. Kwa hivyo, tusiwe na hofu kwamba Bunge la Kitaifa litatupeleka katika njia zisizo haki. Bi. Spika wa Muda, ningependa kuwahimiza Maseneta wenzangu kupambana na Bunge la Kitaifa moja kwa moja kwa sababu Bunge hili ndilo la juu. Itakuwaje tuchaguliwe katika maeneo Bunge mengi na kisha tuogope kusema sisi ndio “Bunge la juu”? Tulipofungua eneo letu la kuegesha magari, nao wakaja hapo. Najua kesho tukifungua chumba chetu cha maankuli watakuja huko pia. Wanatuvamia kila mahali. Kwa hivyo, lazima tulete msimamo ili Bunge la Seneti liwe na majukumu yake na uwezo wake na Bunge la Kitaifa vile vile. Sisi tumetaabika sana kwa kuitwa “Bunge ndogo”. Nangoja kura ije ili tuwaonyeshe nani mdogo. Tusikubali kuwa katika hali hii. Tunapaswa kuangalia na kuutetea ugatuzi. Mwisho, kubadilisha Katiba kwa njia itakayoimarisha Shilingi ya Kenya ndio uzalendo. Kutetea kwamba CDF iwe chini ya Wabunge wa Kitaifa si uzalendo, bali ni The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}