GET /api/v0.1/hansard/entries/591420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591420/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "utoto. Sisi tunataka kuleta uzalendo kwa kuimarisha uwezo wa Seneti. Nilimsikia ndugu yangu, Sen. Murkomen, akisema kwamba wengi wetu hatutakuwa hapa baada ya uchaguzi ujao. Wengi wetu tukakuwa magavana. Kwa hivyo, ingekuwa sisi ni watu ambao mioyo zetu hazijakinai, hatungepigania mageuzi haya bali tungetaka maisha yaendelee vivi hivi. Kwa hivyo, sisi tunafanya hivyo kama Wakenya kwa maana tunaipenda Kenya, na ndio maana tunataka kuhakikisha kuwa tumeweka msingi. Ndugu yangu hapa, Sen. (Dr.) Khalwale, huenda akawa gavana Mungu akimjalia. Hata kama hayuko katika chama kile, mimi nitakwenda pale kwa maana najua kuwa ni mkweli bali si mwizi. Tunajua kuwa sera nyingi zinazoendelezwa katika kaunti zetu ni za wizi na Wakenya wamechoshwa na hali hiyo. Kama mtu si mwizi, inafaa tumpende ziadi na kumkumbatia. Ikiwa Sen. (Dr.) Khalwale hangetaka ugatuzi uendelee, angehakikisha kuwa Seneti halipewi uwezo wowote. Isitoshe, hangetaka magavana wafike ili kujieleza mbele ya Kamati yake. Yeye ndiye amefanya watu waende kortini kwa vile huwaandikia barua akitaka majibu. Kwa hivyo, hangefanya hivyo iwapo alikuwa hataki hayo. Sisi tunafanya mambo kwa imani ya Wakenya. Tunataka ugatuzi na utawala ufanye kazi nchini Kenya. Hatufanyi hivyo kwa vile tunajali maslahi yetu. Leo hii, utapata mtu anataka kutoa Constituencies Development Fund (CDF) na EqualisationFund kutoka kaunti hadi eneo Bunge. Mtu kama huyo anadhani atakuwa Mbunge maisha yake yote? Kwa nini mtu haangalii mbele akafikiria watoto wake, jamii yake na vizazi vinavyokuja? Takwimu zinaonyesha kwamba kila wakati wa uchaguzi, Wakenya huwapeleka nyumbani asilimia 70 ya viongozi waliowachagua. Kwa nini mtu atake pesa ziende kwake? Hajui atapelekwa nyumbani? Kwa hivyo, sisi tuko hapa kuulinda ugatuzi."
}