GET /api/v0.1/hansard/entries/591476/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 591476,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591476/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 758,
        "legal_name": "Boy Juma Boy",
        "slug": "boy-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kunipa nafasi hii ili niungane na Maseneta wenzangu kuunga mkono Hoja hii muhimu. Ukiisoma Hoja hii, unafaa kujiuliza inapendekeza nini. Hoja hii inataka mabadiliko katika Katiba ili kuifanya Seneti hii kuwa na nguvu. Inafaa tujiulize ikiwa ni kweli kwamba Seneti haina nguvu. Jibu la swali hili ni kuwa Seneti haina nguvu. Kwanza tunafaa kuwasifu Wanakamati wa Kamati hii. Kamati hii iliwajumuisha mawakili wanne waliokolea katika taaluma ya uwakili. Nilipotazama vizuri, niliona kuwa ilikuwa na akina dada wawili wazuri sana na walio na elimu ya juu. Ukitazama vizuri, utaona kwamba Kamati hiyo iliundwa na watu walio na busara. Bi. Spika wa Muda, Hoja hii inaazimia kutia nguvu ugatuzi. Tunafaa kujiuliza iwapo ugatuzi katika nchi yetu kulingana na Katiba ya sasa uko hatarini. Ukiangalia vizuri, utapata kuwa ugatuzi uko hatarani. Hii ni kwa sababu ilibidi twende kortini kufuatia Mswada kuhusu Ugawanyaji wa Pesa au Revenue Allocation Bill . Mswada wa pili, ulijulikana kama “Sang Bill.” Mswada huu ulitaka bodi iundwe lakini pia ulikatizwa. Mswada wa tatu uliohusu oversight vilevile ukakataliwa. Tunataka ushahidi gani zaidi ya huo kuonyesha kwamba Seneti hii iko hatarini? Tuko hatarani kwa mujibu wa ushahidi ulioko sasa. Ndio maana niliketi hapa kwa muda mrefu nikisubiri kupewa nafasi ili kuongeza sauti yangu kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ugatuzi ni kitu kizuri sana. Bi. Spika wa Muda, tunafaa kuwasifu wale ambao si wezi lakini majizi ya pesaa za umma yanafaa kulaniwa. Tumeona watu wengine wakinunua likwama moja kwa Kshs109,000. Kama huo si wizi, basi ni nini? Huo ni wizi ulio wazi. Ndio maana tunasema kuwa majizi yalaumiwe kwa wizi na wale wanaofanya kazi vizuri wasifiwe. Ndio maana nasema ya kwamba tuwe na utaratibu na mabadiliko kwa kubadilisha Katiba. Haya hayakuanza leo. Sisi katika mrengo wa the Coalition for Reforms and The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}