GET /api/v0.1/hansard/entries/591479/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591479,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591479/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tuliona mambo haya mapema. Tulianza kampeni za “Okoa Kenya” lakini wenzetu wakatupinga. Leo hii, ni kama kuongeza chumvi katika chakula kwa sababu haya yalikuweko. Hata wewe pia ulikuwa mmojawapo miongoni mwa wale waliokuwa katika mstari wa mbele tulipokuwa tukisema Kenya iokolowe. Tulisema kuwa asilimia ya pesa iliokuwa ikienda kwenya kaunti ni ndogo. Wataalamu na mawakili wa gredi wakiongozwa na Sen. Murkomen na wengine walipokaa, waliona yale yale tuliokuwa tukiyasema sisi. Sasa ndio haya. Hata hivyo, tuwache mambo ya mrengo wa CORD. Tunasema ya kwamba haya maneno si ya leo kwa sababu tulikuwa tumeshayaona. Tulisema kwamba tulihitaji Katiba kubadilishwa, kama si jana, basi kesho. Hii ni kwa sababu Hoja hii imetuwekea hali ambayo itatuondolea unyanyasaji wa Seneti. Maseneta wengi wameeleza hayo lakini unapoenda kwenye kaunti, mfalme mkubwa huko ni bwana mmoja aitwaye gavana na serikali yake ya kaunti. Hata hivyo, gavana hana ujanja kwa sababu lazima pesa za kaunti ziidhinishwe na Seneti ilhali Seneta hana umuhimu kwake. Haya ndio baadhi ya mambo ambayo Hoja hii inahitaji vipengele fulani za Katiba zifanyiwe mabadiliko. Bi. Spika wa Muda, kumekuwa na uoga mkubwa kafuatia swala la kubadilisha Katiba. Umekuwa kama wimbo unaoogopwa watu wanapozungumzia kubadilisha Katiba. Kama walivyosema wengine na Mwenyekiti wa Kamati hii, kuna nchi nyingi ambazo zilipitisha Katiba kama yetu lakini ilibadilishwa baada ya muda fulani. Itabidi sisi, kama Seneti, kuingiza ndani fikra za tatu ama za nne ambazo zina umuhimu katika maswala ya Katiba kwa sababu tumeona upungufu. Waingereza husema, “mvaa kiatu ndiye hujua wapi kinambana sana.” Hata wewe ukivaa kiatu, utajua ni wapi kinakubana. Tunavaa kiatu cha ugatuzi na ndio maana tunahisi kinatubana ndio maana tunasema ya kwamba kuna haja ya Hoja hii kuungwa mkono. Nasisitiza kuwa sisi kama Seneti, bila kutazama mrengo huu au ule, tuiunge mkono Hoja hii kadiri tutakavyoweza na katika fikra moja. Nikinukuu, juzi, Mhe. Rais wa Tanzania alisema kuwa labda uwe mpumbavu ndio hutaelewa. Nimenukuu maneno yake ili mtu asije akasema kuwa Sen. Boy Juma Boy ndiye aliyesema. Nimenukuu mfano ambao ulitolewa na Rais wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akihutubia Bunge juzi. Hakuna Mtanzania mpumbavu. Nikifananisha mfano ule, sifikirii kuna Seneta mpumbavu ambaye atapinga Hoja kama hii kwa sababu ya yale matukio ambayo tunayaeleza, tunayaona na ambayo yako. Bi. Spika wa Muda, marekebisho haya ambayo yameingizwa ndani ya ripoti hii ni ya muhimu sana. Yataweza kutupa mwelekeo mzuri lakini tashwishi yangu kubwa ni umoja wa Seneti. Hivi sasa, tunazungumza kwa lugha moja lakini tuna tabia katika Seneti hii baada ya muda fulani, tukitoka kila mmoja ataegemea kwa msimamo na mrengo wa vyama. Tukitaka kufaulu katika hili, maana tukitoka hapa na utazame utaratibu peke, kutakuwa na swala la referendum. Tukipotea katika laini yetu na kuingia mirengo yetu, basi hatutafaulu. Ukweli wa mambo ni kwamba wako watu ambao haja yao kubwa ni tusifaulu. Wako na wanapenda Seneti isifaulu. Vielelezo vipo kwamba wanapenda tusifaulu na vimeonekana na ushahidi upo kama vile mtu anaposema Matayo 1 na Yohana 2. Ushahidi wa vitendo vya kuonyesha wanavyopenda kuoneka Seneti isifaulu. Si swala la kuzungumzia tu na watu, ushahidi upo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}