GET /api/v0.1/hansard/entries/591481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 591481,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591481/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kutokana na hali hii ndivyo tunasisitiza tuwe na fikira moja na tutoke kwa mirengo ya vyama na tuwe kwa mirengo ya kutazama Seneti kama mlinzi wa ugatuzi na wa kuhakikisha kesho na kesho kutwa Seneti imebaki. Bila Seneti hatuna ugatuzi. Haina haja kuanza kulaumiana. Tusitazame yaliyopita, bali tugange yalimo na yajayo. Nikimaliza kwa kuunga mkono Hoja hii, kikamilivu na kwa dhati wa moyo wangu, kwamba kuna umuhimu wa hii Seneti. Hautajua mpaka utoke hapa na uenda majimboni. Unapofika jimboni, kuna bwana mmoja hubebwa kiti. Bwana huyu ni gavana. Magavana wetu wana magari ya kuwabebea viti na jukwaa ya ugavana. Magari ya kusafirisha viti hivo na jukwa hutumia mafuta ya petrol. Kiti hiki huwa na maadizi haya: County Government of Homa Bay. Hawaongei na zile spika zile mimi na wewe tunatumia, wao wana zao. Haya ndiyo mambo ambayo lazima tuone kwamba mbele yako katika msingi ambayo ni ya kueleweka. Pamoja na uharibifu ambao upo, tukubaliane kwamba ugatuzi ndio nia na jambo ambalo litatuwezesha kuhakikisha Wakenya tutakuwa na nchi moja ya umoja ambayo itatuweka kwa pamoja bila kuwa na wasi wasi, shaka na tashwishi. Bi. Spika wa Muda, hata nikisema sana nitakuwa nachukua nafasi ya wenzangu. Kwa hayo machache, ninashukuru na ninaunga mkono Hoja hii."
}