GET /api/v0.1/hansard/entries/591562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 591562,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591562/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukrani, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono huu Mswada kwa hicho kipengele ambacho kimeletwa na Mhe. Emanikor kwa sababu tumeonyesha wazi kwamba hili Bunge linasimamia kufadhili Katiba yetu na kukubaliana na yote tuliyopitisha. Lakini pia tutaweza kujitenganisha na wale ambao wanataka kufanya mambo yao wakati sisi tunaendesha mambo yetu katika Bunge hususan kama walivyozungumza Waheshimiwa wenzangu. Wakati ule wa nyuma tuliweza kuona wakituletea nguruwe na hali inajulikana wazi kwamba nguruwe si halali kwa Mwislamu. Walitutia katika hali ambayo haikuturidhisha kama Waislamu katika Bunge na hata Kenya nzima. Kwa hivyo, ninaunga mkono."
}