GET /api/v0.1/hansard/entries/592398/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 592398,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/592398/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi ili niunge mkono Hoja hii iliyopendekezwa na Sen. Murkomen. Wakati mwingi majuto ni mjukuu. Sio kwamba hatukujua kwamba kulikuwa na udhaifu kwa Katiba. Haya yalisemwa na wahenga wakati ule lakini sikio la kufa halisikii dawa; hawakusikia. Tunayoyaona leo kuhusu mamlaka ya Seneti ni udhaifu uliotabiriwa kwamba tunaunda Seneti ambayo haitakuwa na mamlaka na kutakuwa na upotevu wa pesa za umma. Sasa imebidi tuanze kufikiria ili tutekeleze yale ambayo tungeyatekeleza jana. Tumefikiria kwamba kura ya maoni ni muhimu wakati huu ambapo Serikali iko taabani, haina pesa. Kura ya maoni ni gharama kubwa. Tuna pengo la deni la zaidi ya Kshs1.3 trilioni. Serikali imeanza kukopa kutoka kwa benki nchini ili kugharamia huduma za kila siku. Sisi tuko na matatizo ambayo yanalenga ukweli na umuhimu ili kuliziba hili pengo ambalo limefanya Serikali na nchi ya Kenya kuwa na shida ambayo tumepata kwa sababu ya udhaifu wa Bunge la Kitaifa. Bunge hili limepitisha Miswaada kiholelaholela bila Seneti kuwajibika, kuangalia na kuchunguza kwa undani na dhati yaliyomo. Umuhimu wa Mswada huu lazima utiliwe maanani. Wakati umefika lazima mamlaka ya Seneti yaangaliwe na yarekebishwe vilivyo kwenye Katiba. Kwa mfano, Kaunti ya Migori imewaka moto sasa hivi. Jana na juzi katika runinga, Spika wa bunge anadaiwa ameiba pesa kiasi cha Kshs12 milioni. Kamati ya Bunge ya Kaunti ya Migori iliketi, ikachunguza na kupata kwamba hela hizo zilitumika vibaya kwa sababu ya Spika. Spika mwenyewe alienda kutafuta vijana kutoka sokoni na kuwajaza Bungeni. Wabunge wa Kaunti walipotaka kuanza kupiga kura, vijana walianza kupiga kelele na Spika akahahirisha Bunge. Bw. Naibu wa Spika, mambo kama hayo yasingekuwa hivyo kama Bunge hili la Seneti lingekuwa na nguvu hata ya kusema: “Bw. Spika, kwa sababu umefanya dhambi kama hiyo, wakati ukichunguzwa kaa kando kwa mujibu wa amri ya Seneta.” Wajua Seneti ina amri hiyo lakini lazima sasa njia ndefu ifuatwe. Mara kupitia petition na haya ni mambo yasiyopendeza. Baada ya Spika huyo kufanya hivyo, aliandaa msafara mrefu kupita miji yote katika Kaunti ya Migori akijitukuza kana kwamba amefanya jambo nzuri sana. Haja hii inaipa Seneti nguvu za kuangalia uteuzi, sio wa Mawaziri tu bali pia viongozi wa tume mbalimbali, kabla ya kupewa wajibu huo. Hizi ni tume muhimu ambazo uteuzi wao si wa kiholelaholela. Lazima usomwe, uangaliwe na aliyeteuliwa achunguzwe na wazee wa Seneti. Tuliitwa “Jumba la wazee” na sio tusi wala kosa kwa sababu ni Bunge lililojaa watu wenye hekima. Kwa mfano, lazima Seneti hii iangalie ni nani huyu ambaye atahudumu kama mwangalizi wa mambo ya kaunti au hata mkuu wa polisi. Serikali ikitaka kuenda vitani, Seneti hii iangalie ni kwa nini. Kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Serikali ikitaka kutumia jeshi kufanya kazi ya polisi, Seneti iamue. Ni kwa sababu hapa kuna watu walio na kipawa cha umri na wala sio kukimbilia mambo, kuyasema na kuyatelekeleza bila kufikiria na kujua undani wake. Ninaomba Seneti hii ipewe uwezo wa kutekeleza hayo yote. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}