GET /api/v0.1/hansard/entries/592400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 592400,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/592400/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, sasa hivi mimi na ndugu zangu tunakaa tu kama kuku aliye na pua wazi lisilo na kifuniko na chochote chaweza kuingia. Bunge la Seneti! Hata huna uwezo wa kutekeleza wajibu wako hata tu kufanya mkutano. Huwezi kuitisha kikao cha viongozi wote wa kaunti ukae nao siku mbili au tatu mchambue mipango ya maendeleo ambayo inahitaji kufadhiliwa. Kazi ya kuombaomba utafika nayo wapi? Tunahitaji hela zitakazowekwa wakfu na Serikali ili kuhakikisha kwamba Seneta ana uwezo wa kutekeleza wajibu wake mashinani. Huo ndio ukweli. Lakini sasa yatatendeka vijijini na wewe ukiwa Seneta utayasikia tu. Hata unatumia gari lako kwa sababu huna gari la Serikali na labda umetoka katika kaunti kubwa. Kama mimi hapa, Migori nina maeneo Bunge nane. Utoke Kusini, Kaskazini, Magharibi hadi Mashariki, utakuwa umetumia petroli na tairi umemaliza kiasi gani na pesa kutoka kwa mfuko wako? Kule vijijini pia kuna ombaomba ilhali mshahara wako ni ule ule tu. Haiwezekani kwa sababu hata ukiwa mzuri sana, kuna wakati ambapo unaishiwa, unarudi na kuketi kitako kisha mambo yanaharibika vijijini. Kwa hivyo, Hoja hii sio tu kuangalia wajibu wa Seneti kwa uteuzi wa viongozi kadha wa kadha, lakini unataka pia Seneti ipewe uwezo wa kuamua mambo muhimu kwa Bajeti. Juzi, Bunge la Kitaifa lilipitisha Bajeti kubwa ya Kshs2.3 trilioni kiholela tu bila kujua hela hizo zitatoka wapi. Tunasikia tu:“Tunataka kufanya hivi.”Barabara na reli zinajengwa huku, viongozi wanaruka kwa ndege huku na huku, magari makubwa yanatumika na ndege zinapaa kushoto na kulia. Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Hela zimekwisha kwa sababu pia midomo imekuwa mingi. Mirija imewekwa ndani kwa sababu Seneti haina uwezo wa kukata mirija hiyo. Hamna nguvu. Hela zimekwisha na sasa ni kutapatapa kama kipofu na upofu utafika nao wapi ukitaka kuongoza nchi? Sasa ni kilio kushoto na kulia; madaktari huko wanalia kwamba hawalipwi mishahara yao, hakuna dawa hospitalini, polisi hawana mafuta ya magari yao na hata Bunge linakatiwa umeme. Juzi Mbunge mmoja amelalamika kwamba hata hakuna maji ya kujitawaza chooni. Bunge la taifa! Aibu! Kuna viongozi 349 waliochaguliwa katika Bunge la Kitaifa na 67 katika Seneti na haya yanapita katikati ya vidole bila kuonekana. Bw. Naibu wa Spika, ni kwa sababu sheria ilichujwa hadi Seneti ikakosa uwezo. Seneti iliyaona haya wakati Bajeti ilipoletwa ndani ya Bunge tukiangalia tu na wengine tukasononeka. Tukauliza hata hela za kushughulikia zahanati au hospitali kubwa, lakini hatukupata.Tuliwauliza watenge Kshs10 bilioni tu zishughulikie hospitali za Level 5 lakini walikataa kusikia. Walipitisha Kshs3 bilioni tu na sasa hospitali zimekwama. Ni wehu! Wamejazwa na uwehu wa nguvu za Katiba ambayo ina dosari na lazima irekebishwe. Lazima hela zitafutwe kwa hima. Katiba ilivyo sasa hivi, haitatupeleka mbali. Lazima Seneti ipewe uwezo wake wa kuongoza nchi hii kusudi jambo likitendeka katika Bunge la Kitaifa, likifika kwa Seneti tutaliangalia, tuliangazie mawazo yetu na kuona hili halifai wala halitekelezeki. Hili ni shimo kuu la kuvunja umma kusudi na wao pia wasituambie basi walimbuke. Tunawaambia, limbukeni, mwamke kutoka usingizini. La sivyo, basi, Jumba la Seneti halistahili kuwepo. Hakuna budi basi tuseme Bunge la Seneti livunjwe kama ilivyokuwa zamani. Kwa sababu halina nguvu, haina haja kuwa na Seneti. Kama nikuketi hapa kuangalia mambo yakiharibika, huna uwezo, mwishowe unakula mshahara mwisho wa mwezi, huwezi hata kufika uko mashinani ukatekeleza wajibu wako kwa sababu hamna vifaa vya kufanya hivyo, basi livunjwe. Livunjwe kwa sababu laongeza utumizi wa mapato ya Serikali. Livunjwe na maeneo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}