GET /api/v0.1/hansard/entries/593912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 593912,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/593912/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, nampa hongera Sen. Khaniri kwa kuleta jambo hili. Kitambulisho ni stakabadhi muhimu sana. Kule Kilifi, kuna vitambulisho vingi sana ofisini kwa chifu. Watu wetu hawajui pa kuvipeleka vitambulisho hivyo au labda watu hawana akaunti za benki au uajiri. Kamati hii ni lazima ihakikishe kwamba vitambulisho hivyo vimepewa wenyewe. Najua wengi wetu wataenda kuvitafuta kura itakapowadia. Kama kawaida, sisi huenda mbio dakika ya mwisho kutafuta stakabadhi za kutumia kupiga kura."
}