GET /api/v0.1/hansard/entries/594394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 594394,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/594394/?format=api",
    "text_counter": 207,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuunga mkono Mswada huu. Kwanza, ningependa kumpongeza Mhe. Neto kwa kuuleta Mswada huu Bungeni ili tuwe na sheria ya kuhifadhi vyema stakabadhi za kiafya. Stakabadhi za kiafya ni muhimu sana na zinastahili kutunzwa vilivyo.Vile vile, itakuwa vyema ikiwa stakabadhi hizi zitahifadhiwa katika mitambo ya kisasa, kiasi cha kwamba mgonjwa akiwa ameagizwa kwenda kwa matibabu zaidi katika hospitali nyingine, kuwe na njia ya kuwezesha stakabadhi zile zisafirishwe moja kwa moja, bila kumtumia mgonjwa mwenyewe, bali,ziingie katika mitambo ya hospitali ile nyingine ambapo mgonjwa atahudumiwa zaidi. Hii inafanyika hata kwa nchi jirani, Tanzania. Kuna wakati mmoja nilienda kutibiwa Arusha, na sikuwa na haja ya kutembea na kadi kutoka kwa afisa mmoja hadi afisa mwingine. Ni mitambo tu inayotumika. Ukifika kule habari zako zishafika na unahudumiwa vilivyo pasipo na kuhangaika na kubeba makaratasi. Mhe. Naibu Spika Wa Muda, hakika ni vyema kuhudumiwa na stakabadhi zako kuwekwa na watu ambao wamehitimu vile ambavyo sasa kutakuwa na halmashauri ambayo itakuwa inasimamia uelimishaji wa wafanyikazi. Hilo litakuwa ni jambo la busara, maana watakaoshughulikia stakabadhi za kiafya ni watu ambao watakuwa wamehitimu kisawasawa."
}