GET /api/v0.1/hansard/entries/594522/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 594522,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/594522/?format=api",
    "text_counter": 119,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, nimesimama kulipinga tengenezo badilisho hili ambalo Mhe. Korir amependekeza. Nalipinga kwa sababu hatutaki kuwa tunakaa tukingoja maafa yatokee ili tuyashughulikie. Tunataka tuzuie maafa. Kama itakuwa silaha zifuatiliwe popote zilipo, ni lazima kuwe kumewekwa mikakati. Polisi, jeshi ama kitengo chochote kile cha usalama kinapaswa kuwa na mikakati ya kufuatilia mahali ambako silaha ziko. Hatutaki kungojea mpaka shida itokee ndiyo tuanze kutapatapa. Nina imani kwamba tukiingiza pesa katika hali ambayo imepangiwa na kusitokee mambo ya ufisadi, tutaweza kuokoa maisha ya Wakenya mahali popote walipo, kuliko vile ambavyo hali iko. Hivi sasa, pesa zinatumika lakini haieleweki zinatufaidi vipi, ilhali watu wanapoteza maisha yao. Katika maeneo ya ufugaji, kila asubuhi, kuna watu ambao hujitengenezea bunduki. Je, bunduki hizo nazo tuziache? Ni lazima kuwe na mikakati ambayo itatumika kuzitafuta na kutambua mahali ziko. Kama mtu ana bunduki ambayo haikuandikishwa na kujumuishwa kwenye mpangilio huo, ichukuliwe kwamba yeye ni mhalifu. Tusipitishe tengenezo badilisho The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}