GET /api/v0.1/hansard/entries/594545/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 594545,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/594545/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kabla niseme jambo, ningependa kusema kuwa mmesalimiwa na watu wangu wa Ruiru na wakaniambia muendelee kushikilia Serikali ya Jubilee ambayo ni ya kusema na kutenda. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningetaka kuunga mkono lakini kabla nifanye hivyo, ningependa kusema watu wengi wana bunduki. Ni vizuri kuongea juu ya bunduki lakini mwananchi akisikia bunduki, anaona kifo ama madharau. Hiyo ni kwa sababu wakati mwingi, hata wale wana bunduki za halali wanafikiria ni nguo ya kitenge ama koti ya pesa nyingi. Wanaonyesha kila mtu kuwa wana bunduki. Tumefika mahali hata mtu akienda kula kwa hoteli pale mashinani, halipi! Mwenye hoteli akimudai pesa, anatoa bunduki na kuiwekea mezani. Kwa hivyo, hata kama tunataka kujua mahali bunduki ziko, ningeomba kwa heshima, hata wale wako nazo kihalali, waweze kuzitumia kwa njia nzuri. Kuna wengi ambao wako nazo na wanazitumia vibaya. Wengine wanaibia wale walionazo kihalali. Ningeomba ikiwa tutajua mahali ziko, ni vizuri kwa sababu tukiweka mashini ile, kila mtu atajua. Hii itasaidia polisi wetu kwa sababu wakati mwingi katika maeneo Bunge yetu, wakati kumekuwa na ukora kwa nyumba fulani, ni vigumu sana kujua kama mtu ako na bunduki halali, ama amejitengenezea ile ya mbao ya kupiga ngeta. Kwa hivyo, nikiunga mkono, ni vizuri tuweze kujua bunduki ngapi tulizonazo ni halali. Tukiendelea hivyo, usalama utaweza kuwa katika nchi yetu ya Kenya. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}