GET /api/v0.1/hansard/entries/594697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 594697,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/594697/?format=api",
"text_counter": 79,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Bw. Spika, ninafikiri nimelijibu vizuri. Nimesema ningelieleza kwamba haimo katika mawazo yangu kwamba kuna yeyote anaweza kununulika. Lakini kama amelielewa kimakosa, basi wacha nimuweke katika hali ya usawa kwamba asiwe na taswishi. Naona Kiswahili hapo kimeeleweka. Nimeliondoa tamshi hilo. Kwa hali hiyo, naiunga mkono Kamati hii na ningependa kusisitiza kwamba nimehudumu katika moja ya Kamati hizi; zina kazi nyingi, zina muda mrefu, zina muda ambao wakati mwingine Kamati zinafika mpaka usiku wa manane, kwa hivyo, ni kazi ya kujitolea. Kwa hayo machache, naunga mkono. Asante."
}