GET /api/v0.1/hansard/entries/595376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595376,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595376/?format=api",
"text_counter": 378,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika. Naomba nitoe mchango wangu kwa Mswada huu ambao umekuja wakati huu. Naunga mkono Mswada huu ijapokuwa kuna mapendekezo mengi muhimu ambayo yanahitajika katika Mswada huu ili unufaishe watu wa nchi hii. Kama tunavyojua, mafuta yamepatikana katika pembe nyingi za nchi. Mara nyingi watu ambao wanaishi karibu na maeneo ambapo rasilimali kama hii zimepatikana ndio wanaokuwa hawana chochote na hawawezi kujimudu, huku mafuta yakitolewa na kusafirishwa. Wale ambao wanapata faida ya mafuta hayo sio wenyeji wanaoishi mahali pale. Wenyeji wa maeneo hayo utawakuta hawana namna ya kuishi. Mapendekezo yangu wakati tutakapokuwa tunatoa marekebisho ni angalau jambo hili lishughulikiwe ili Mswada huu uweze kuwatambua wenyeji ili nao wanufaike na ile rasilimali ambayo imepatikana. Jambo lingine la kusikitisha ni mara nyingi utakuta nchi hii imegawanywa katika sehemu mbalimbali na watu wamezikimbilia wakazifunga na kusema ni zao. Unakuta Wizara inawapatia kibali kuwa waendelee kushikilia sehemu hizo kama ni zao. Wao ndio wameshikilia mafuta au mawe mengine ya thamani na watu wengine ambao wanahitaji kupatiwa nafasi ya kuchimba chochote ambacho kiko chini ya ardhi wananyimwa kwa sababu mna watu wamepeleka maombi wakapatiwa eneo fulani. Utakuta watu wamezibana sehemu hizo na hawazitumii bali wamezishikilia wakiwa wanangoja wakati utakaofaa wapate kuziuza. Ukweli wa mambo ni kwamba walikimbilia kwa Wizara, wakapatiwa na wakazishikilia. Jambo lingine la kero sana ni mamlaka ambayo amepewa Waziri kushughulikia suala la kupeana vibali vya kuchimbua mafuta ama kuangalia rasilimali. Mamlaka haya ni mengi na wanaweza kuyatumia vibaya. Ni ombi langu kuwa wakati tutakapokuwa tumekaa hapa kama Wabunge tukiangalia vile tutakavyoleta marekebisho katika Mswada huu, jambo hili litazingatiwa ili mamlaka hayo yapunguzwe na tubuni kitengo ambacho kitashughulikia suala hili. Mara nyingi tumeona kwamba mamlaka haya yakiwa na mtu mmoja yanatumiwa vibaya na mara nyingi hayatumiwi kwa manufaa ya nchi. Jambo lingine ambalo naomba liangaliwe ni utata mwingi ambao hutokea sana wakati rasilimali imepatikana. Watu huzozana na kugombana kwa sababu mipaka yao haijatambuliwa. Hivi sasa utaona nchi yetu ya Kenya iko na utata na Somalia. Hii ni kwa sababu ya rasilimali zilizoko pale nje. Hebu tujiulize, huu utata unaletwa na nini? Kila mtu anataka kujua mali iliyo pale chini ni ya nani."
}